Sunday, February 15, 2015


Sera ya Elimu na Mafunzo
SERA YA ELIMU NA MAFUNZO
2014
i
Sera ya Elimu na Mafunzo
ii
Sera ya Elimu na Mafunzo
YALIYOMO
VIFUPISHO v
DIBAJI vii
SURA YA KWANZA 1
1.0. UTANGULIZI 1
1.1. Hali Ilivyo 8
SURA YA PILI 18
2.0. UMUHIMU WA SERA 18
2.1. Dira, Dhima na Malengo ya Sera 19
SURA YA TATU 21
  1. 3.0.  HOJA NA MATAMKO YA SERA 21
  2. 3.1.  Mfumo, miundo na taratibu nyumbufu kumwezesha 21 Mtanzania kujiendeleza kwa njia mbalimbali katika mikondo ya kitaaluma na kitaalamu
  3. 3.2.  Elimu na mafunzo yenye viwango vya ubora 24 unaotambulika kikanda na kimataifa na kukidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa
3.3 Upatikanaji wa fursa mbalimbali za elimu na 40 mafunzo nchini
  1. 3.4.  Mahitaji ya Rasilimaliwatu kulingana na Vipaumbele 46 vya Taifa
  2. 3.5.  Usimamizi na uendeshaji madhubuti wa elimu na 50 mafunzo nchini
  3. 3.6.  Mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu na 55 mafunzo nchini
  4. 3.7.  Mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia 57 masuala mtambuka.
iii
Sera ya Elimu na Mafunzo
URA YA NNE 60 4.0. MUUNDO WA KISHERIA 60 4.1. Utangulizi 60 4.2. Sheria za kusimamia elimu na mafunzo 60 SURA YA TANO 62 5.0. MUUNDO WA KITAASISI 62 5.1. Utangulizi 62 5.2. Ngazi ya Taifa 63 5.3. Ngazi ya Mkoa 65 5.4. Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa 65 5.5. Ngazi ya Kata 66 5.6. Ngazi ya Shule na Vyuo 67 5.7. Ufuatiliaji na Tathmini 67 5.8. Hitimisho 68
iv
Sera ya Elimu na Mafunzo
VIFUPISHO
AZAKI Asasi za Kiraia
CA Continuous Assessment
International Growth Centre – Presidents’ Office Planning Commission
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania
MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
IGC-POPC MKUKUTA
MMES MMEJU
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Elimu ya Juu
MMEU Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi
Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa
Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii
OWM- Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na TAMISEMI Serikali za Mitaa
SADC Southern Africa Development Community TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
MEMKWA MUKEJA
UNESCO
United Nations Educational, Scientific and Cultural Organisation
UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini
URT United Republic of Tanzania
WyEMU Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi VVU Virusi vya Ukimwi
v
Sera ya Elimu na Mafunzo
vi
Sera ya Elimu na Mafunzo
DIBAJI
Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia lengo hili, mfumo wa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa za kutosha kwa watu kujielimisha. Hali kadhalika, mfumo huu unawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalika na kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kufanikisha hili, Serikali imekuwa ikitekeleza sera mbalimbali, hususan, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimumsingi (2007) na kuwa na mafanikio mbalimbali. Hata hivyo, katika kipindi hicho, changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo udhaifu katika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhaba wa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na changamoto katika ithibati na uthibiti wa ubora wa shule na vyuo katika ujumla wake vimechangia katika kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo nchini.
Sera hii imebainisha masuala ambayo Serikali, kwa kushirikiana na wadau katika elimu na mafunzo, itayawekea mkazo zaidi ili kuweka mazingira mazuri ya kufikia malengo ya mipango ya maendeleo. Masuala haya ni pamoja na kuinua ubora wa mfumo wa elimu na
vii
Sera ya Elimu na Mafunzo
mafunzo ili uwe na tija na ufanisi, kuendelea kutoa fursa za elimu na mafunzo kwa usawa na kuendelea kuinua ubora wa mitaala ya elimu na mafunzo ili ikidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa. Aidha, Serikali itaendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Alama, pamoja na lugha nyingine za kigeni katika elimu na mafunzo. Vilevile, itaendelea kuinua ubora wa mfumo wa upimaji, tathmini na utoaji vyeti katika ngazi zote. Serikali itaimarisha uwezo wa uongozi na utawala katika sekta ya elimu na mafunzo na kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo.
Sera hii mpya inaweka Dira ya elimu na mafunzo nchini kuwa ni “Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa” na Dhima yetu kuwa ni “kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu”. Ili kufanikisha utekelezaji wa Sera hii kwa ukamilifu, kunahitajika ushiriki wa wadau wote wa elimu na mafunzo katika ngazi zote, ikiwemo sekta binafsi, Asasi za Kiraia (AZAKI) na washirika wengine wa maendeleo.
Mwisho, napenda kuwashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika mchakato mzima wa kukamilisha Sera hii.
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
viii
Sera ya Elimu na Mafunzo
SURA YA KWANZA
1.0. Utangulizi
Sera hii ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ni matokeo ya kuhuishwa na hatimaye kufutwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimu Msingi (2007). Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu; na utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimu Msingi (2007) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni. Mwaka 2006, Serikali ilibadilisha muundo wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kujumuisha elimu ya juu na baadaye mwaka 2008 kujumuisha elimu ya ufundi katika wizara hiyo. Sera hizo za elimu, kwa ujumla, zilitoa mwongozo kuhusu kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi; kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa usawa; kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo; kuhuisha muundo wa uongozi wa elimu kwa kupeleka madaraka na majukumu katika ngazi ya shule, jamii, wilaya na mikoa; kuinua ubora wa elimu; kuimarisha uhusiano kati ya elimu rasmi na elimu nje ya mfumo rasmi na kuwezesha ukuaji wa utamaduni wa elimu ya kujiajiri na kubuni ajira.
Katika miaka 19 ya utekelezaji wa Sera ya kwanza ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 pamoja na Sera nyingine mahususi za elimu na mafunzo, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu. Mafanikio haya ni pamoja na kupanua wigo wa elimu katika ngazi zote, kuanzia elimu ya awali hadi
1
Sera ya Elimu na Mafunzo
elimu ya juu. Kwa mfano, kwa kutumia taarifa zilizopo za miaka mbalimbali, idadi wa watoto wanojiunga na elimu ya awali imeongezeka kutoka asilimia 24.7 mwaka 2004 hadi 37.3 mwaka 2013 na kiwango cha watoto walioandikishwa katika elimu ya msingi imeongezeka kutoka asilimia 77.6 mwaka 1995 hadi asilimia 96.2 mwaka 2013. Kiwango cha watoto wanaojiunga na elimu ya sekondari kimeongezeka pia kutoka asilimia 14.6 mwaka 1995 hadi 59.5 mwaka 2013.
Hali kadhalika, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi imeongezeka kutoka 4,641 mwaka 2000/01 hadi 145,511 mwaka 2012/13. Aidha, elimu ya juu imepanuka ambapo vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki vimeongezeka kutoka chuo 1 mwaka 1995 hadi 50 mwaka 2013 na kuwezesha idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu kwa ngazi ya Shahada kuongezeka kutoka 16,727 mwaka 2000/01 hadi 162,510 mwaka 2012/13.
Utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo ulifanyika kupitia sheria, kanuni, miongozo pamoja na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu iliyoandaliwa mwaka 1997. Kupitia program hiyo, uliandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJ) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (MMEU). Pia kulikuwa na mipango na programu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Kupitia sheria, kanuni, miongozo na mipango hii, fursa za elimu na mafunzo zimeongezeka katika ngazi zote; ugatuaji wa majukumu katika sekta ya elimu na mafunzo umefanyika kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa; vyombo vya ithibati na uthibiti wa ubora wa
2
Sera ya Elimu na Mafunzo
elimu na mafunzo ya ufundi, elimu ya vyuo vikuu, mfuko wa elimu na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu pia vimeanzishwa na vinafanya kazi nzuri ya kuendeleza elimu na mafunzo nchini.
Hata hivyo, changamoto nyingi zimejitokeza katika kipindi cha utekelezaji wa Sera hizi, ambazo zimekuwa zikiathiri ubora na usawa katika elimu inayotolewa kwenye ngazi mbalimbali. Changamoto hizi ni pamoja na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vitabu, maabara, maktabana madarasa;. upungufu wa walimu hususan walimu wa sayansi, hisabati na stadi za kusoma, kuhesabu na kuandika; kushuka kwa morali ya kufundisha miongoni mwa walimu kwa sababu ya maslahi yasiyoridhisha na mazingira magumu ya kazi; utambuzi hafifu wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu na mazingira duni ya kujifunzia; kutokuwepo kwa utaratibu wa utambuzi na uendelezaji wa wanafunzi wenye vipaji na vipawa; matumizi hafifu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji wa elimu na mafunzo; na walimu na wanafunzi kutomudu lugha ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi mbalimbali za elimu. Vilevile kiwango cha watu wazima wenye kufahamu kusoma, kuandika na kuhesabu kimeshuka kutoka asilimia 85 mwaka 1992 hadi asilimia 77.9 kulingana na Sensa ya Taifa ya mwaka 2012.
Aidha, bado Sekta ya elimu na mafunzo inakabiliwa na changamoto ya mfumo usiokidhi mahitaji ya elimu na mafunzo nchini. Mfumo wa elimu na mafunzo umetawaliwa na muundo wa kitaaluma wenye dhana ya kuchuja wahitimu ili kupata wachache wenye uwezo mkubwa katika taaluma na watakaosoma hadi kumaliza katika ngazi ya chuo kikuu. Hali hii inatokana na nafasi za elimu na mafunzo ngazi za juu kuwa
3
Sera ya Elimu na Mafunzo
chache kadri wanafunzi wanavyohitimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na kuendelea, hivyo kuwa na muundo wa kuchuja badala ya ule wa kutoa fursa kulingana na uwezo, vipaji na vipawa. Hali kadhalika, muundo wa 2+7+4+2+3+ unachukua jumla ya miaka 18 kutoa rasilimaliwatu. Hii ina maana kwamba mwanafunzi anayeanza masomo akiwa na umri wa miaka 7 atamaliza elimu ya juu akiwa na umri wa takribani miaka 23. Umri huu ni mkubwa ikilinganishwa na nchi nyingine kama za Afrika ya Kusini, Maurishasi, Malesia na Ufini ambapo umri wa kijana anayemaliza elimu ya juu ni takribani miaka 20 hadi 22. Vilevile, hakuna mwingiliano fanisi kati ya muundo wa elimu ya ufundi na muundo wa elimu ya jumla na hivyo kushindwa kuwawezesha wahitimu wa elimu ya ufundi kujiendeleza katika elimu ya juu. Pamoja na hayo, kuna ukosefu wa mfumo endelevu wa utambuzi wa sifa mbadala utakaowawezesha watu waliopata ujuzi kwa njia mbalimbali za elimu na mafunzo kujiendeleza kielimu na kuingia katika ulimwengu wa kazi.
Vilevile, kumekuwa na changamoto katika kuinua ubora wa elimu na mafunzo kutokana na mitaala katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo kutokidhi mahitaji ya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na teknolojia na hivyo kutoa wahitimu ambao hawana umahiri wa kutosha kuhimili ushindani katika ulimwengu wa kazi. Aidha,Taasisi na mashirika yanayotoa huduma za kielimu yaliyopo chini ya Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo yana mamlaka kamili ya uendeshaji wa shughuli za elimu bila kuwa na mahusiano ya kisheria katika utendaji baina yao na wizara zinazosimamia elimu na mafunzo na hivyo kuathiri ubora wa elimu itolewayo. Hali kadhalika, changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa ugharimiaji endelevu kutokana na mifuko ya
4
Sera ya Elimu na Mafunzo
elimu kutokidhi mahitaji ya elimu katika ngazi zote na hivyo kuhitaji vyanzo vingine vya ugharimiaji endelevu wa elimu na mafunzo.
Utekelezaji wa Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) kuhusu ugatuaji umekuwa na changamoto mbalimbali. Katiba inatamka katika Sura ya Nane (kuhusu madaraka kwa umma), kwamba, madhumuni ya kuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi na hivyo kuwezesha Serikali za Mitaa kuwajibika kutekeleza kazi zake katika eneo husika. Sheria za Serikali za Mitaa zinatoa majukumu kwa Halmashauri kuhusu elimu katika Kifungu cha 55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ya 1982. Ni kwa mantiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Matangazo ya Serikali Na. 494 na 494A ya mwaka 2010 aligatua na kuiweka katika usimamiaji wa OWM-TAMISEMI elimu ya awali, msingi na sekondari na kuacha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushughulikia Sera katika masuala yote ya elimu na mafunzo. Hata hivyo bado kuna changamoto za muingiliano wa baadhi ya majukumu katika utekelezaji wa ugatuaji kwa upande wa utendaji na usimamiaji wa elimu kati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI.
Katika miaka ya hivi karibuni, viwango vya ubora wa elimu vimekuwa vikishuka. Hali hii inadhihirishwa na ufaulu katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na elimu ya sekondari ngazi ya kawaida kuwa na mserereko wa kushuka kutoka asilimia 54 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 31 mwaka 2012, kwa upande wa elimu ya msingi; na asilimia 90 mwaka 2007 hadi asilimia 43 mwaka 2012 kwa elimu ya sekondari; wakati idadi ya watahiniwa inaongezeka mwaka hadi mwaka. Maarifa na Ujuzi wa wahitimu katika ngazi hizo ni mdogo
5
Sera ya Elimu na Mafunzo
ikilinganishwa na ngazi ya elimu waliyofikia. Hali kadhalika, maarifa na ujuzi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi na elimu ya juu havikidhi mahitaji mbalimbali katika ulimwengu wa kazi. Tathmini zinaonyesha kwamba, ili kuimarisha ubora na ufanisi wa elimu na mafunzo nchini, kuna ulazima wa kuimarisha maeneo mbalimbali ambayo yanahusika na ubora wa elimu na mafunzo.
Katika harakati za kimaendeleo, yapo mabadiliko ya sera za kijumla na mipango ya kitaifa iliyojitokeza katika kipindi cha utekelezaji wa sera hizi. Kutokana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Muda mrefu 2011/12 hadi 2024/25, Serikali imelenga kujenga jamii iliyoelimika na yenye kupenda kujielimisha. Pamoja na azma hiyo, Tanzania imeridhia Itifaki ya SADC (1997) kuhusu elimu na mafunzo inayozitaka nchi wanachama kuwa na elimumsingi ya lazima kwa kipindi kisichopungua miaka tisa; Itifaki ya Dakar (2000) kuhusu Elimu kwa wote; Makubaliano ya Perth UNESCO (2007) kuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia na mafunzo ya ufundi na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, kuna baadhi ya masuala mtambuka yakiwemo mazingira, jinsia, VVU na UKIMWI na Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambayo yamejitokeza na yanahitaji kujumuishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo.
Sekta ya elimu na mafunzo ina jukumu la kuandaa na kuzalisha rasilimaliwatu kwa ajili ya Taifa. Ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba kuna nakisi kubwa ya wataalamu walioelimika kwa kiwango cha elimu ya juu wanaohitajika ili Tanzania ifikie kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Taarifa ya IGC- POPC (2011) inaonyesha kuwa, Rasilimaliwatu ya Tanzania, kwa kiasi kikubwa, ni wafanyakazi wenye ujuzi wa chini ambao
6
Sera ya Elimu na Mafunzo
ni asilimia 84, wakifuatiwa na wenye ujuzi wa kati ya asilimia 13 na wenye ujuzi wa juu asilimia 3. Hata hivyo, kwa nchi za kipato cha kati ngazi ya chini, ulinganifu unaonyesha kuwa nchi hizo zina wastani wa asilimia 55 ya wafanyakazi wenye ujuzi wa chini, asilimia 33 ujuzi wa kati na asilimia 12 ujuzi wa juu. Hivyo, sekta ya elimu na mafunzo ina changamoto ya kuinua mchanganyiko wa wafanyakazi wenye ujuzi katika fani mbalimbali ili kufikia mahitaji ya rasilimaliwatu kwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Mfumo wa elimu na mafunzo wa sasa una changamoto ya kuliwezesha Taifa kukidhi ongezeko la mahitaji ya rasilimaliwatu kulingana na vipaumbele vya Taifa kwa sababu takwimu za elimu za mwaka 2000 hadi 2012, zinaonyesha kuwa ni wastani wa asilimia 5 tu ya wahitimu wa darasa la saba ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi kufikia elimu ya sekondari ya juu; na wastani wa asilimia 4 tu ya wahitimu hao wa darasa la saba ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi elimu ya juu. Kwa mwenendo huo ni dhahiri kwamba Taifa litaendelea kuwa na nakisi ya wataalamu kama hatua madhubuti za kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu hazitachukuliwa.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imeandaliwa ili kutoa mwelekeo wa elimu na mafunzo nchini kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia na changamoto za elimu na mafunzo kitaifa, kikanda na kimataifa, ili kuongeza fursa, ufanisi na ubora wa elimu na mafunzo nchini na kufikia viwango vya rasilimaliwatu kwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
7
Sera ya Elimu na Mafunzo
1.1. Hali Ilivyo
Uchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, umeonyesha kuwa matamko 59 kati ya matamko 149 ya Sera hayakutekelezwa. Kati ya hayo, matamko 25 yalihusu elimu ya msingi na sekondari, 18 yalihusu elimu ya ufundi na 16 yalihusu elimu ya juu. Tathmini ilibaini pia kuwa mpango mkakati wa kuelekeza utekelezaji wa sera hizo haukuandaliwa mpaka mwaka 1997 ulipoanzishwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, na mwaka 2001 ulipoandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Tathmini ilibaini pia kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa na wilaya unafanywa na mamlaka mbalimbali zinazoongozwa na kanuni na taratibu tofauti pamoja na OWM-TAMISEMI. Walimu wanaandaliwa na kuajiriwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati haki zao za kiutumishi na nidhamu zinashughulikiwa na Idara ya Utumishi wa Walimu. Utaratibu huu wa usimamizi wa walimu chini ya mamlaka tatu tofauti unafanya hali ya uwajibikaji na utawala bora kuwa mgumu. Kutokana na taarifa ya tathmini, inapendekezwa kuwa Serikali iunde Bodi ya kitaalamu ya kusimamia maendeleo ya utaalamu wa ualimu. Vilevile walimu wawe chini ya mwajiri mmoja atakayeshughukia masuala ya ajira, nidhamu na maendeleo yao.
Vyuo vya elimu ya ufundi stadi na vyuo vya ualimu havikuwekewa muundo wa kitaasisi unaoviunganisha na maafisa elimu wa wilaya na mikoa kama ilivyoelekezwa kwenye Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995. Taasisi zilizo chini ya Wizara zinazotoa huduma za kielimu hazina uhusiano wa kiutendaji
8
Sera ya Elimu na Mafunzo
katika utekelezaji wa majukumu yao kati ya taasisi na taasisi na uhusiano wa moja kwa moja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na OWM-TAMISEMI. Katika tathmini hiyo ilipendekezwa kuwa kiundwe chombo kitakachokuwa na wajibu wa kuratibu na kuhakiki ubora wa mitaala, upimaji, utoaji vyeti na tuzo, ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu ya msingi na sekondari.
Uchambuzi wa tathmini hiyo ulibaini kwamba kuna umuhimu wa kupunguza miaka ya kupata elimu ya awali kutoka miaka miwili hadi mwaka mmoja, na kupunguza umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa miaka mitano badala ya miaka saba. Muundo wa elimu wa sasa wa 2+7+4+2+3+ pamoja na kwamba ulionekana kuwa umelisaidia Taifa hadi tulipofikia, huchukua muda mrefu tangu mwanafunzi anapoanza elimu ya msingi mpaka anapohitimu chuo kikuu. Tathmini pia ilibaini kuwa elimu inayotolewa katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari imeegemea zaidi kwenye mkondo wa taaluma hivyo kupunguza uwezo wa kubaini vipaji na vipawa vya wanafunzi na kuviendeleza katika stadi nyingine nje ya taaluma. Tathmini hiyo ilipendekeza kuwa na muundo wa 1+6+4+2+3+ ambao mhitimu atamaliza mzunguko wa masomo kwa muda mfupi; na mikondo ya ufundi ijumuishwe kwenye elimu ya msingi na sekondari. Utambuzi wa watoto wenye vipaji na vipawa ufanyike mapema katika elimu ya awali na msingi ili waendelezwe katika ngazi zinazofuata.
Tathmini pia ilionyesha kuwa mitaala ya baadhi ya vyuo haina ulinganifu katika maudhui na muda wa mafunzo kwa programu zinazolingana na kufanana. Aidha, maudhui ya mitaala ya ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo hayakidhi mahitaji ya jamii na ya ulimwengu wa kazi. Katika fursa za
9
Sera ya Elimu na Mafunzo
elimu na mafunzo Serikali, sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo, wamekuwa wakichangia kuongeza fursa kwa makundi yote kwa usawa.
Hali kadhalika, tathmini ilionyesha kuwa jitihada za Serikali zimeleta mafanikio ya kuongezeka kwa fursa katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Hata hivyo, kumekuwa na changamoto ya wanafunzi kuacha shule kutokana na sababu mbalimbali na wengi kutopata fursa ya kuendelea kutokana na ufaulu mdogo.
Vile vile, taasisi kama vile Taasisi ya Elimu Tanzania, Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania huratibu ithibati na uthibiti wa viwango vya ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali. Kila taasisi ina bodi ya utendaji ambayo hutoa maamuzi kuhusu masuala ya utoaji na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika maeneo ya mamlaka zao. Tathmini ilibaini kuwa taasisi hizi zinahitaji muunganiko fanisi wa utendaji kazi kisheria ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa ubora wa elimu na mafunzo nchini.
1.1.1 Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995
Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ulifanyika kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES). Baadhi ya malengo ya Sera yaliyotekelezwa katika mipango hiyo ni:
10
Sera ya Elimu na Mafunzo
  1. (i)  Kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu na mafunzo kwa kuhimiza kuanzisha na kuendesha shule na taasisi za elimu na mafunzo,
  2. (ii)  Kutilia mkazo utoaji wa elimu bora kwa kuangalia upya mitaala, kuinua ubora wa usimamizi wa walimu na kutumia maendeleo ya mwanafunzi ya kila siku katika upimaji,
  3. (iii)  Kupanua upatikanaji wa fursa za elimu kwa kuzingatia usawa kwa makundi yote nchini, na
  4. (iv)  Kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo kwa kudhibiti matumizi ya Serikali pamoja na kuhimiza uchangiaji wa gharama.
Katika kutekeleza mipango hiyo, kumekuwa na mafanikio yakiwemo kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi katika kutoa elimu na mafunzo, kuimarishwa kwa usimamizi wa walimu kwa kuundwa chombo cha kushughulikia masuala ya walimu kama vile usajili, kuthibitishwa kazini, kupandishwa madaraja na masuala ya nidhamu. Aidha, kumekuwa na mafanikio katika maandalizi, uendelezaji, utoaji na ufuatiliaji na tathmini ya mitaala ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu. Hali kadhalika, kumekuwa na ongezeko la fursa mbalimbali katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu. Idadi ya wanafunzi walioandikishwa katika elimu ya msingi iliongezeka kutoka 3,942,888 (wavulana 1,992,739 na wasichana 1,950,149) mwaka 1996 hadi 8,247,172 (wavulana 4,086,280 na wasichana 4,160,892) mwaka 2012 ambayo ni ongezeko la zaidi ya mara mbili. Kwa upande wa elimu ya sekondari ngazi ya kawaida, kumekuwa na ongezeko la wanafunzi walioandikishwa kutoka 185,119 (wavulana 98,435
11
Sera ya Elimu na Mafunzo
na wasichana 86,684) mwaka 1996 hadi wanafunzi 1,802,810 (wavulana 954,961 na wasichana 847,849) mwaka 2012 ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara tisa. Aidha, Idadi ya wanafunzi katika elimu ya sekondari ya juu imeongezeka kutoka 13,974 (wavulana 9,597 na wasichana 4,377) mwaka 1996 hadi wanafunzi 81,462 (wavulana 55,512 na wasichana 25,950) mwaka 2012 ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara tano. Mafanikio haya pamoja na mengine yamechangiwa na utaratibu wa Serikali kutoa ruzuku kwa shule za umma za msingi na sekondari. Aidha, wazazi na wanafunzi wameendelea kuchangia ada na michango mbalimbali katika shule za sekondari na vyuo kadri wanavyohitajika kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu za elimu na mafunzo.
Mafanikio hayo yamekuwa pia na changamoto katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya mitaala kutokidhi mahitaji kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na teknolojia. Vilevile, kutokana na upanuzi wa fursa za elimu katika ngazi zote kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya nyenzo, vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote.
1.1.2 Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996
Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996 ilitekelezwa kupitia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya utoaji wa elimu katika sekta ya ufundi. Hata hivyo, kupitia Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, uliandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Pamoja na masuala mengine, Sera ya Elimu ya Ufundi na
12
Sera ya Elimu na Mafunzo
Mafunzo ilikuwa na malengo yafuatayo:
(i)
(ii)
(iii) (iv)
(v) (vi)
Kupata idadi ya kutosha ya mafundi na wanateknolojia mahiri ili kukidhi mahitaji ya sekta rasmi na isiyo rasmi;
Kuanzisha na kuimarisha taasisi za mafunzo ya ufundi kwa kuziwekea vitendea kazi na wataalamu ili kutimiza malengo;
Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uendeshaji na ugharimiaji wa elimu ya ufundi;
Kuwa na mfumo fanisi na bora wa elimu na mafunzo ya ufundi ili kuleta usawa wa fursa za elimu na mafunzo;
Matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi; na
Kuhimiza na kuratibu ubora wa matokeo ya wahitimu kupitia uanzishwaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi.
Utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996 umeleta mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kukamilika kwa mfumo wa sifa linganifu za mafunzo ya ufundi na ufundi stadi kutoka ufundi mchundo hadi uhandisi; kutekelezwa kwa mtaala unaozingatia umahiri wa stadi hususan kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi; kujumuishwa kwa masomo ya stadi za kazi katika mitaala ya elimu ya msingi; kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi kwa sheria ya Bunge Sura ya 129; na kuongezeka kwa vyuo vya ufundi kutoka 695 mwaka 2005 hadi 750 mwaka 2012 na kuwezesha ongezeko la wanachuo kutoka 78,586 (wanaume 43,022 na wanawake
13
Sera ya Elimu na Mafunzo
35,564) mwaka 2005 hadi wanachuo 104,440 (wanaume 54,350 na wanawake 50,190) mwaka 2012. Vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi viliongezeka kutoka vyuo 195 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 260 mwaka 2011 na kuongeza udahili wa wanachuo kutoka 39,759 (wanaume 30,123 na wanawake 9,636) mwaka 2005 hadi 85,040 (wanaume 46,342 na wanawake 38,698) mwaka 2011.
Pamoja na mafanikio hayo, utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulikuwa na changamoto zifuatazo:
  1. (i)  Ukuaji mdogo wa fursa za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ukilinganishwa na mahitaji ya taifa na ulimwengu wa kazi;
  2. (ii)  Mtazamo hasi kuhusu mafunzo ya ufundi;
  3. (iii)  Fikra mgando za ujinsi katika dhana nzima ya mafunzo ya ufundi;
  4. (iv)  Upungufu wa wakufunzi wenye sifa na kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya kuwabakisha kazini;
  5. (v)  Kutokuwepo kwa mwingiliano fanisi kati ya mfumo wa elimu ya ufundi na mfumo wa elimu ya jumla; na
  6. (vi)  Mafunzo kutokidhi mahitaji ya ulimwengu wa kazi.
14
Sera ya Elimu na Mafunzo
1.1.3 Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999
Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999, ilikuwa na malengo ya kuongeza fursa za elimu ya juu na kuweka sheria, kanuni na miongozo ya kuunda vyombo vya kuimarisha ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu ya juu.
Katika utekelezaji wa malengo hayo, Sheria ya Vyuo Vikuu Sura ya 346, Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Sura 178 na Sheria ya Mfuko wa Elimu Sura 412, zilitungwa. Kufuatia kutungwa kwa Sheria hizi, Tume ya Vyuo Vikuu, iliundwa kwa ajili ya kusimamia ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu ya juu. Aidha, Mamlaka ya Elimu Tanzania na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilianzishwa ili kuwezesha upatikanaji wa fedha na mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini. Utendaji wa vyombo hivyo kwa pamoja, umechangia fursa za elimu ya juu kuongezeka ambapo idadi ya vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki iliongezeka kutoka 20 mwaka 2005 hadi vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki 50 mwaka 2013 na kuongeza udahili wa wanachuo kutoka 37,667 (wanaume 25,061 na wanawake 12,606) mwaka 2005 hadi 162,510 (wanaume 105,381 na wanawake 57,129) mwaka 2013 ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara nne.
Pamoja na mafanikio hayo, kumekuwa na upungufu katika maeneo yafuatayo:
(i) Kutokuwa na mwingiliano wa kutosha na endelevu wa elimu unaowezesha wahitimu wa elimu ya sekondari na ufundi kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu na hivyo kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi katika elimu ya juu;
15
1.2
Sera ya Elimu na Mafunzo
  1. (ii)  Kutokuwepo kwa ugharimiaji endelevu wenye kuleta tija na hivyo kuendelea kuwa mzigo mkubwa kwa Serikali, wazazi na wanafunzi;
  2. (iii)  Kutokuwepo kwa ushirikiano bayana baina ya sekta ya elimu na viwanda katika utoaji wa elimu ya juu;
  3. (iv)  Kutokuwa na mfumo endelevu na mpana wa utambuzi wa sifa mbadala unaoruhusu wahitimu katika ngazi mbalimbali za elimu kujiunga na elimu ya juu;
  4. (v)  Kuendelea kuwepo kwa vikwazo mbalimbali ikiwemo mitazamo hasi inayokwamisha maendeleo ya elimu ya juu, ufinyu wa rasilimali mbalimbali na matumizi duni ya TEHAMA katika maendeleo ya elimu ya juu; na
  5. (vi)  Baadhi ya mitaala ya elimu ya juu kutotosheleza mahitaji ya maendeleo ya Taifa na ulimwengu wa kazi.
Changamoto za jumla katika Sekta ya Elimu na
Mafunzo Nchini
Utekelezaji wa sera za elimu na mafunzo, unakabiliwa na changamoto mbalimbali za jumla zikiwemo:
  1. (i)  Kukosekana kwa mfumo nyumbufu unaoruhusu elimu na mafunzo kupatikana na kutambulika kwa njia mbalimbali mbadala;
  2. (ii)  Kuwepo kwa elimu na mafunzo yenye viwango vya ubora visivyotambulika kitaifa, kikanda na kimataifa;
16
Sera ya Elimu na Mafunzo
  1. (iii)  Kutokuwa na mfumo wa ajira unaowezesha upatikanaji wa wataalamu wa kada mbalimbali wanaohitajika katika sekta ya elimu na mafunzo nchini;
  2. (iv)  Kukosekana kwa fursa zitolewazo kwa kila Mtanzania kulingana na mahitaji yake na sehemu na mazingira aliyopo;
  3. (v)  Kutokuwa na mfumo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo wenye wigo mpana na endelevu;, na
  4. (vi)  Kutozingatia masuala mtambuka kikamilifu katika elimu na mafunzo.
17
Sera ya Elimu na Mafunzo
SURA YA PILI 2.0. UMUHIMU WA SERA
TangukuanzakutekelezwakwaSerayaElimunaMafunzo(1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia ambayo yameleta changamoto na kuzifanya Sera hizo zipitwe na wakati. Mabadiliko ya kiuchumi duniani yameleta msukumo kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea ama kubadilisha au kuimarisha sera, programu na mikakati yake ili ziweze kuhimili ushindani wa kiuchumi na kuleta maendeleo endelevu ya kijamii, kisayansi na kiteknolojia. Tanzania ni moja ya nchi ambazo uchumi wake umeendelea kukua na kufikia asilimia 7 mwaka 2012. Kukua huku kunatokana na kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi. Azma ya Tanzania ni kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo sekta ya elimu na mafunzo imepewa jukumu la kuandaa rasilimaliwatu ya kutosha kwa ajili ya kukidhi mabadiliko hayo.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ililenga elimu ya msingi na ya lazima iwe miaka 7, lakini kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ni kuwa na taifa la watu wenye elimu ya kati na ya juu ili kuwa na watendajikazi wenye uwezo wa kushughulikia kikamilifu changamoto za kimaendeleo. Hali kadhalika, Sera ya Ajira na Utumishi wa Umma ya mwaka 1999 inatamka kuwa sifa ya kuajiriwa katika utumishi wa umma kwa masharti ya kudumu ni kiwango cha elimu kisichopungua elimu ya sekondari ya kidato cha nne.
18
Sera ya Elimu na Mafunzo
Ushirikiano wa Tanzania na nchi nyingine kikanda na kimataifa umeleta msukumo wa kurekebisha Sera ili kuzingatia masuala ya ushirikiano na utangamano. Masuala hayo ni pamoja na Kuoanisha mitaala; Ulinganifu wa viwango vya elimu na mafunzo; Upimaji na utoaji tuzo; Kutokomeza kutojua kusoma na kuandika pamoja na ulinganifu wa sifa za kujiunga na vyuo vya elimu na mafunzo; na kuleta ulinganifu wa mifumo ya elimu na sifa za wahitimu kikanda. Pia, kwa kuwa Tanzania siyo kisiwa, Sera hii inajikita katika kuimarisha utangamano katika elimu na mafunzo ili kumjengea Mtanzania ujuzi, umahiri na uwezo wa kukabiliana na mahitaji yanayojitokeza katika ulimwengu wa kazi na maisha kwa ujumla.
2.1. Dira, dhima na malengo ya sera
Msingi wa elimu na mafunzo utajikita katika kumjengea Mtanzania misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi, umahiri na kumwezesha kujitegemea. Elimu ya kujitegemea itaendelea kuongoza utoaji wa elimu na mafunzo kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika jamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.
2.1.1. Dira
Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
2.1.2. Dhima
Kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu.
19
Sera ya Elimu na Mafunzo
2.2. Malengo ya Sera
2.2.1. Lengo la Jumla:
Kuwa na Watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya Taifa na kuhimili ushindani.
2.2.2. Malengo Mahsusi
Malengo mahsusi ya Sera ni kuwa na:
  1. (i)  Mfumo, miundo na taratibu nyumbufu kumwezesha
    Mtanzania kujiendeleza kwa njia mbalimbali katika mikondo ya kitaaluma na kitaalamu;
  2. (ii)  Elimu na mafunzo yenye viwango vya ubora unaotambulika kitaifa, kikanda na kimataifa;
  3. (iii)  Upatikanaji wa fursa mbalimbali za elimu na mafunzo nchini;
  4. (iv)  Ongezeko la rasilimaliwatu kulingana na vipaumbele vya Taifa;
  5. (v)  Usimamizi na uendeshaji madhubuti wa elimu na mafunzo nchini;
  6. (vi)  Mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo nchini; na
  7. (vii)  Mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia masuala mtambuka.
20
Sera ya Elimu na Mafunzo
SURA YA TATU 3.0. HOJA NA MATAMKO YA SERA
3.1. Mfumo, Miundo na Taratibu Nyumbufu Kumwezesha Mtanzania Kujiendeleza kwa Njia Mbalimbali katika Mikondo ya Kitaaluma na Kitaalamu.
Suala
Mfumo wa elimu na mafunzo
Maelezo
Serikali imejitahidi katika kufanikisha upatikanaji wa haki ya elimu kwa watoto wa jinsi zote kwa kuwezesha uandikishaji kufikia asilimia 105.5 ya wanafunzi katika elimu ya msingi. Hata hivyo, elimu baada ya elimu ya msingi imeendelea kuwa na changamoto mbalimbali kwa sababu mfumo uliopo sasa unategemea zaidi utaratibu wa kuchuja wanafunzi kwa ajili ya kuendelea na masomo badala ya kutoa fursa ya kuwaendeleza kadri ya uwezo, vipaji na vipawa vyao. Mfumo huu pia umejikita katika taaluma na ulibuniwa wakati shule na vyuo vikiwa vichache na ulilenga zaidi dhana ya kusoma na kumaliza katika ngazi ya chuo kikuu na hivyo kuwafanya wale wanaoshindwa kuendelea kitaaluma kuchaguliwa kujiunga na elimu na mafunzo ya ufundi stadi au mafunzo ya ufundi. Hiki ni kiashiria cha mfumo kushindwa kutoa fursa anuai za elimu na mafunzo ambazo zingeweza kumfanya mhitimu apate ujuzi na maarifa kwa ajili ya ulimwengu wa kazi.
Hali kadhalika, kwa muundo wa elimu yetu wa 2+7+4+2+3+ mwanafunzi anayeanza masomo akiwa na umri wa miaka 7 atamaliza elimu ya juu akiwa na umri mkubwa, takribani miaka 23 ikilinganishwa na nchi kama za Afrika ya Kusini, Maurishasi,
21
Sera ya Elimu na Mafunzo
Malesia na Ufini ambapo umri wa kijana anayemaliza elimu ya juu ni takribani miaka 20 hadi 22. Kwa mantiki hii, mfumo nyumbufu unahitajika ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomaliza katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo kuendelea na masomo katika ngazi nyingine.
Lengo
Kuwa na mfumo nyumbufu wa elimu na mafunzo wenye tija na ufanisi na hivyo kuongeza idadi ya wananchi walioelimika na kuwa na maarifa kwenye fani mbalimbali.
Tamko
3.1.1 Serikali itaweka mfumo nyumbufu katika elimu na mafunzo ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kujielimisha na kuwa huru kutafuta elimu katika fani wanayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wao.
Suala
Umri wa elimumsingi na muda wa elimu na mafunzo
Maelezo
Muundo wa elimu na mafunzo uliopo unatoa fursa ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano kujiunga na elimu ya awali kwa muda wa miaka miwili. Mtaala wa elimu ya awali umeandaliwa kwa namna ambayo unatakiwa ufundishwe kwa miaka 2 lakini Tathmini ya Sera za Elimu na Mafunzo ya mwaka 2008 inaonesha kuwa mtaala huo unaweza kufundishwa kwa mwaka mmoja kama ukifundishwa kwa ufanisi. Pia, Itifaki ya Dakar ya mwaka 2000 ambayo ilitakiwa itekelezwe hadi ifikapo mwaka 2015 ambayo Tanzania imeridhia na kufuatana na UNESCO (ISCED, 1997), elimu ya awali inatakiwa kutolewa kwa watoto
22
Sera ya Elimu na Mafunzo
wenye umri kati ya miaka mitatu hadi sita.
Kwa sasa, Elimu ya Msingi inatolewa kwa miaka saba (7) na ni ya lazima kwa uandikishaji na mahudhurio kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Sura ya 353 ya sheria za Nchi. Wahitimu wa elimu ya msingi katika mfumo wa sasa wanakuwa na umri wa miaka 13. Baadhi ya wahitimu huendelea na elimu ya sekondari na mafunzo ya ufundi; waliokosa fursa hizo huingia kwenye ulimwengu wa kazi. Wahitimu hawa wanakuwa na umri mdogo na hawana maarifa na ujuzi unaotosheleza kujiunga na ulimwengu wa kazi au kukabiliana na changamoto za maendeleo, iwapo watakosa fursa ya kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya kawaida au elimu ya ufundi. Shirika la Kimataifa la Kazi limeweka mkataba wa umri wa chini wa kuajiriwa kwa baadhi ya kazi kuwa ni miaka 15. Hali kadhalika, Itifaki ya SADC (1997) kuhusu elimu na mafunzo inasisitiza kutokomeza kutojua kusoma na kuandika kwa kuweka juhudi ya kuwa na elimumsingi na ya lazima kwa wote angalau kwa kipindi kisichopungua miaka tisa (9). Kutokana na makubaliano haya, kuna umuhimu wa kurekebisha muundo wa elimu ya awali na msingi ya sasa ili elimu ya awali iwe ya lazima na itolewe kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kulingana na mahitaji ya mwanafunzi husika. Kila mtoto mwenye umri wa miaka 4 hadi 6 na ambaye amepata elimu ya awali, kwa mujibu wa sheria, apatiwe elimumsingi itakayotolewa kwa muda wa miaka 10 ili kumwezesha mwanafunzi kusoma, kuandika na kuhesabu, kuwa na ufahamu wa mambo ya ujumla na kupata maarifa na ujuzi katika elimu, ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
Lengo
Kurekebisha muda wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali ili kuleta tija, ufanisi na matumizi bora ya rasilimali.
23
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.1.2. Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa ya lazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
3.1.3. Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kuanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.
3.1.4. Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo wa Taifa.
3.1.5. Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumo wa umma inatolewa bila ada.
3.2. Elimu na Mafunzo Yenye Viwango vya Ubora Unaotambulika Kikanda na Kimataifa na Kukidhi Mahitaji ya Maendeleo ya Taifa
Suala
Uthibiti wa ubora wa elimu na mafunzo
Maelezo
Ubora wa elimu na mafunzo unatokana na ubora wa mitaala iliyopo, umahiri wa watekelezaji wa mitaala hiyo, uongozi,
24
Sera ya Elimu na Mafunzo
usimamiaji, mazingira ya kutolea elimu na mafunzo, tathmini na rasilimali zilizopo. Taifa kwa sasa linakabiliwa na changamoto mbalimbali katika suala la ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi zote.
Matokeo katika mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne yamekuwa na mserereko wa kushuka kutoka asilimia 54 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 31 mwaka 2012 kwa upande wa elimu ya msingi; na asilimia 90 mwaka 2007 hadi asilimia 43 mwaka 2012 kwa elimu ya sekondari, wakati idadi ya watahiniwa inaongezeka mwaka hadi mwaka. Maarifa na Ujuzi wa wahitimu katika ngazi hizo ni mdogo ikilinganishwa na ngazi ya elimu waliyofikia. Halikadhalika, maarifa na ujuzi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi na elimu ya juu hayakidhi mahitaji mbalimbali katika ulimwengu wa kazi. Tathmini zinaonyesha kwamba, ili kuimarisha ubora na ufanisi wa elimu na mafunzo nchini, kuna ulazima wa kuinua ubora wa mitaala, ukaguzi wa shule, tathmini, ithibati, na mamlaka zinazohusika na masuala hayo.
Idara ya ukaguzi wa shule ina jukumu la kufuatilia ubora wa elimu ya msingi na sekondari kwa kuzingatia mitaala na viwango vilivyowekwa. Utendaji wa idara hii umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Changamoto hizo ni pamoja na kuendelea kutumia falsafa ya ukaguzi iliyokuwa na tija wakati shule zikiwa chache tofauti na sasa ambapo shule ni nyingi na hivyo kuhitaji ushirikishwaji zaidi wa wadau na mbinu mbadala; upungufu katika muundo wa usimamizi na uendeshaji wa ukaguzi wa shule ambao umewaweka wakaguzi mbali na shule ziliko pamoja na kushindwa kuzifanya Kamati na Bodi za Shule, Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule pamoja na
25
Sera ya Elimu na Mafunzo
wazazi kuwajibika vya kutosha katika suala la usimamizi na uthibiti wa ubora wa elimu itolewayo na shule zetu. Ukaguzi hafifu pia unachangiwa na kutokuwa na wataalamu mahiri na wa kutosha na ukosefu wa vitendea kazi.
Kwa upande mwingine, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi lina jukumu la kuratibu ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu katika vyuo vya elimu ya ufundi; na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ina jukumu la kuratibu ithibati na uthibiti wa ubora wa mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo mbalimbali vya ufundi stadi. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imepewa majukumu ya kuweka na kuratibu ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu ya juu katika vyuo vikuu nchini. Utendaji wa vyombo hivi vya ithibati pamoja na vyombo vingine kama Taasisi ya Elimu Tanzania, Bodi ya Huduma za Maktaba, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Mamlaka ya Elimu Tanzania umekuwa na changamoto katika kuinua viwango vya ubora wa elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo, vyuo vya ufundi stadi na vyuo vikuu. Uhusiano baina ya taasisi hizi na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na OWM-TAMISEMI ni mdogo kwa kuwa hakuna utaratibu madhubuti wa uratibu baina yao. Sheria za vyombo hivi zinahitaji kutathminiwa upya ili kuleta mshikamano katika mfumo mzima wa usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.
Lengo
Kuwa na ufanisi katika uratibu, usimamizi, ithibati na uthibiti wa ubora katika utoaji wa elimu na mafunzo.
26
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.2.1. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaimarisha usimamizi, ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi zote.
3.2.2. Serikali itahakikisha vyombo vya usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo vinahusiana kiutendaji katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
3.2.3. Serikali itaimarisha mfumo, mbinu, dhana na falsafa ya ukaguzi wa shule ili kuleta ufanisi zaidi katika uthibiti wa ubora wa elimumsingi nchini.
Suala
Mitaala ya elimu na mafunzo
Maelezo
Mtaala ni mwongozo wa elimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo ambao ikiwa hautaandaliwa vizuri, kutekelezwa ipasavyo au kutathminiwa kwa umakini, mfumo wa elimu utashindwa kufanya kazi na hautaweza kuleta matarajio yanayokusudiwa na jamii. Hadi mwaka 2005 mitaala iliyokuwepo kwa upande wa elimu ya awali, msingi na sekondari ilijikita zaidi katika maudhui ya ufahamu na kuwa na msisitizo mdogo katika kujenga ujuzi. Kuanzia mwaka 2005 mitaala hiyo ilibadilika na kuwa ya kujenga ujuzi. Tathmini inaonyesha kuwa mabadiliko haya yalifanyika bila kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walimu, wazazi, waajiri, wanafunzi, wakufunzi, wahadhiri, vyama vya kitaalamu, vyama vya kisiasa, taasisi za kidini, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, waratibu wa elimu na wakaguzi. Aidha, hapakuwa na maandalizi ya kutosha kwa watekelezaji wa mitaala. Hivyo,
27
Sera ya Elimu na Mafunzo
walimu kwa ujumla hawafundishi kwa namna iliyotegemewa katika mitaala iliyopo.
Baadhi ya mitaala ya ngazi za ufundi, ufundi stadi na elimu ya juu imepitwa na wakati na haikidhi mahitaji ya ulimwengu wa kazi na hivyo wahitimu wa mitaala hiyo kutoajirika au kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi pale wanapoajiriwa. Pia, kumekuwa na changamoto kwa wahitimu waliomaliza masomo katika mtaala wa ufundi kutotambulika kujiunga na mtaala wa taaluma kwa baadhi ya fani; au mhitimu aliyemaliza katika mtaala wa taaluma kutotambulika katika mtaala wa ufundi.
Tathmini pia zinaonesha kuwa mitaala ya baadhi ya vyuo haina ulinganifu katika maudhui na muda wa mafunzo kwa programu zinazolingana na kufanana. Kwa mantiki hii, kuna umuhimu wa kufanya tathmini ya mitaala iliyopo ili kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji ya elimu na mafunzo ya sasa na ya baadaye kuendana na mahitaji ya maendeleo na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kitaifa, kikanda na kimataifa.
Lengo
Kuwa na mitaala yenye tija, iliyofanisi na inayokidhi mahitaji ya soko la ajira katika kuleta maendeleo ya Taifa na kuhimili ushindani.
Tamko
3.2.4. Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itahuisha mitaala iliyopo katika ngazi zote za elimu na mafunzo ili iende na wakati na kukidhi mahitaji ya elimu na mafunzo ya sasa na siku zijazo kwa kuzingatia mahitaji ya Taifa, walengwa na soko la ajira.
28
Sera ya Elimu na Mafunzo
3.2.5. Serikali, kwa kushirikiana na wadau, itahakikisha mitaala inazingatia stadi za msingi za mawasiliano, kusoma, kuandika na kuhesabu; kutafiti; kuchambua taarifa; kutafsiri, kutathmini na kutumia maarifa, uvumbuzi, ubunifu na ujasiriamali katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
3.2.6. Serikali itaimarisha usimamiaji na upimaji wa utekelezaji wa mitaala katika taasisi za elimu na mafunzo katika ngazi zote, ili kuleta ufanisi wa elimu na mafunzo yatolewayo.
Suala
Elimu ya Sayansi na Teknolojia
Maelezo
Elimu ya Sayansi na Teknolojia ni muhimu katika kumwezesha mwananchi kumudu mazingira yake na kumwezesha kuchangia maendeleo ya taifa. Watoto huanza kufundishwa somo la sayansi kuanzia darasa la III na katika elimu ya sekondari ngazi ya kawaida wanafunzi wote husoma Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati hadi kidato cha pili (2). Aidha, wanafunzi wote huendelea kusoma Baiolojia na Hisabati hadi kidato cha nne (4). Baadhi ya wanafunzi huchagua kuendelea na masomo ya Fizikia na Kemia kuanzia kidato cha tatu (3) hadi cha nne (4). Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wanafunzi 100 ni wanafunzi kati ya 30 – 35 tu ambao wanasoma masomo ya sayansi katika kidato cha tatu (3) na nne (4) ambao wakifaulu ndiyo wanaotarajiwa kusomea fani mbalimbali za Sayansi na Teknolojia katika vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo.
Mitaala ya elimu ya msingi na sekondari inatakiwa kuweka
29
Sera ya Elimu na Mafunzo
mkazo katika elimu ya Sayansi na Teknolojia. Makubaliano kuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia (UNESCO-PERTH 2007) yanasisitiza kufanya mapitio ya mitaala ya elimu ya Sayansi na Teknolojia ili kuongeza hamasa ya wanafunzi kutambua umuhimu wa Sayansi na Teknolojia katika jamii. Pia kuna umuhimu wa kuweka mkazo katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kufundishia na kujifunzia.
Lengo
Kuwa na idadi ya kutosha ya wananchi walioelimika katika Sayansi na Teknolojia na kukidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa.
Tamko
3.2.7. Serikali itaimarisha muundo na utaratibu wa ufundishaji wa masomo ya Hisabati, Sayansi na Teknolojia katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
3.2.8. Serikali itahakikisha matumizi zaidi ya Sayansi na Teknolojia katika utoaji wa elimu na mafunzo katika ngazi zote.
Suala
Nyenzo, vifaa, zana na mbinu za kufundishia na kujifunzia
Maelezo
Utekelezaji fanisi wa mitaala unategemea upatikanaji wa nyenzo, vifaa na zana stahiki za kufundishia na kujifunzia kulingana na mahitaji ya masomo na programu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Nyenzo, vifaa, na zana hizo ni pamoja na mihtasari, vitabu vya kiada na ziada, kemikali za maabara, mitambo na karakana. Kumekuwa na upungufu wa nyenzo, vifaa na zana bora za kufundishia na kujifunzia katika
30
Sera ya Elimu na Mafunzo
ngazi zote za elimu na mafunzo ambapo, kwa mfano, uwiano wa kitabu kwa wanafunzi katika elimu ya msingi ni takribani kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (3) na kati ya wanafunzi wanne (4) hadi tisa (9) kwa shule za sekondari kulingana na somo. Pia, baadhi ya vifaa, zana na nyenzo zilizopo, ama zimepitwa na wakati au haziendani na mahitaji ya sayansi na teknolojia ya sasa. Hali hii imekuwa ikichangia kudhoofisha utoaji wa wahitimu bora.
Vilevile, mfumo huria wa uchapishaji wa vitabu na uandaaji wa zana na nyenzo nyingine za elimu na mafunzo umeathiri upatikanaji wa vitabu, zana na nyenzo bora na za kutosha katika shule na vyuo nchini. Pia, gharama za vitabu, zana na nyenzo husika imekuwa kubwa kuliko uhalisia wa gharama hizo. Katika hali ya aina hii, ni muhimu kuweka utaratibu mahususi wa upatikanaji wa vitabu, zana na nyenzo bora na za kutosha zinazokidhi mahitaji.
Lengo
Kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.
Tamko
3.2.9. Serikali itahakikisha vifaa, nyenzo na zana stahiki za kufundishia na kujifunzia katika elimu na mafunzo zinatosheleza kulingana na mahitaji na maendeleo ya sayansi, teknolojia na mbinu za kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote.
3.2.10. Serikali itahakikisha upatikanaji wa kitabu bora kimoja cha kiada kwa kila somo kwa kila mwanafunzi katika elimumsingi ambavyo vitaandaliwa kwa utaratibu maalumu.
31
Sera ya Elimu na Mafunzo
3.2.11. Serikali itatoa na kusimamia matumizi ya kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo katika elimumsingi ili kufanikisha upimaji wa matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu.
Suala
Miundombinu katika taasisi za elimu na mafunzo.
Maelezo
Miundombinu iliyopo katika shule, vyuo na taasisi nyingine za elimu na mafunzo ni pamoja na majengo, mifumo ya maji, umeme na barabara. Miundombinu hii imechakaa na haitoshelezi mahitaji kwa makundi yote ambapo katika elimu ya msingi kuna upungufu wa asilimia 49 kwa madarasa, asilimia 79 kwa nyumba za walimu, asilimia 49.1 kwa madawati na asilimia 60 kwa vyoo. Elimu ya sekondari, kuna upungufu wa asilimia 25 madarasa na asilimia 77 kwa nyumba za walimu. Kuwepo kwa miundombinu ya kutosha na yenye viwango vya ubora stahiki ni muhimu katika kuinua ubora wa elimu na mafunzo katika ngazi zote. Mipango ya maendeleo ya elimu na mafunzo iliyopo haitoshelezi mahitaji ya miundombinu kulingana na ongezeko la watumiaji. Aidha, kunahitajika kujenga utamaduni wa utunzaji na uhifadhi, ukarabati na ukarafati wa miundombinu ya taasisi za elimu na mafunzo.
Lengo
Kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia
Tamko
3.2.12. Serikali itahakikisha kuwepo kwa miundombinu bora na stahiki ya kutosheleza mahitaji ya elimu na mafunzo
32
Sera ya Elimu na Mafunzo
kwa makundi yote katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
Suala
Mazingira salama na huduma muhimu shuleni na vyuoni.
Maelezo
Mazingira katika baadhi ya shule na vyuo nchini ni duni na hayana usalama wa kutosha. Takwimu kwa upande wa shule za sekondari zinaonyesha kuwa ni shule 3,415 kati shule 4,528 zenye huduma ya umeme. Zipo changamoto nyingi katika upatikanaji wa huduma bora na muhimu kama chakula, maji safi na salama, afya, umeme, mawasiliano na usafiri. Huduma hizi huchangia kuongeza ushiriki kwa walimu na wanafunzi katika mchakato wa elimu na mafunzo. Mazingira tulivu, salama na yenye kuvutia walimu na wanafunzi huongeza tija katika ufundishaji na ujifunzaji. Kuna umuhimu wa kuwa na mazingira yanayokidhi mahitaji na huduma muhimu shuleni na vyuoni ili kuinua ubora wa elimu na mafunzo.
Lengo
Kuwa na mazingira salama na huduma muhimu na endelevu shuleni na vyuoni.
Tamko
3.2.13. Serikali itahakikisha kuwa huduma muhimu zikiwemo za chakula bora, mawasiliano, umeme, maji safi na salama, na afya zinapatikana katika shule na vyuo.
3.2.14. Serikali itahakikisha kuwepo kwa mazingira bora na yenye usalama katika utoaji wa elimu na mafunzo nchini.
33
Sera ya Elimu na Mafunzo
Suala
Ushauri na unasihi katika elimu na mafunzo.
Maelezo
Katika shule za msingi, sekondari na vyuo, huduma ya ushauri na unasihi haitolewi kama huduma ya msingi kwa wanafunzi. Huduma hii hutolewa na walimu wa malezi na nidhamu ambao pia siyo wataalamu wa ushauri na unasihi na huwajibika kufundisha masomo mbalimbali hali ambayo inasababisha huduma hiyo kutotolewa kwa ufanisi. Kukosekana kwa ufanisi katika utoaji wa huduma hii shuleni na vyuoni, kumechangia kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Huduma ya ushauri na unasihi inalenga kumwezesha mwanafunzi na jumuiya ya shule na chuo kwa ujumla kukabiliana na changamoto za maisha, ili kujenga mwelekeo, tabia na kuendeleza mila, desturi na maadili mema katika jamii. Pia, huduma hii inahitajika katika kumsaidia mwanafunzi kujua mustakabali wa masomo atakayoyachagua au aliyoyachagua na umuhimu wake katika maendeleo yake na ya Taifa.
Vilevile, ushauri na unasihi unahitajika kwa wafanyakazi katika ngazi zote za elimu ili waweze kupata stadi za maisha za kujitambua na kufanya maamuzi sahihi katika kutekeleza wajibu wao kikamilifu kama walezi wa wanafunzi na jamii.
Lengo
Kuwa na huduma ya ushauri na unasihi inayokidhi mahitaji katika elimu na mafunzo.
Tamko
3.2.15. Serikali itaimarisha utoaji wa huduma ya ushauri na unasihi katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
34
Sera ya Elimu na Mafunzo
Suala
Elimu yenye kudumisha amani.
Maelezo
Utandawazi, tofauti za kiuchumi na mwingiliano wa watu wenye tamaduni mbalimbali umechangia katika kuleta mabadiliko ya maadili na tabia na hivyo kuleta changamoto za amani katika jamii. Elimu katika taifa ni mhimili wa kudumisha amani katika jamii kwa kujenga stadi za kutatua migogoro, kujenga umoja wa kijamii na mshikamano. Kuna umuhimu wa kuwa na elimu ya amani itakayolenga kuwasaidia wanafunzi kupata uwezo wa kuzuia na kutatua migogoro kwa amani wakati inapotokea miongoni mwa watu, kati ya watu au baina ya makundi, kitaifa au kimataifa. Mitaala ya elimu na mafunzo iandaliwe kwa kuzingatia haki na kujenga Taifa lenye amani na utulivu.
Lengo
Kuwa na mhitimu mwenye stadi za kudumisha amani, kuhimili na kutatua migogoro katika jamii.
Tamko
3.2.16. Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha stadi za kudumisha amani, kuhimili na kutatua migogoro, uzalendo na maadili zinajumuishwa katika mitaala ya elimu na mafunzo kwa ngazi zote.
Suala
Matumizi ya Kiswahili, Kiingereza, lugha nyingine za kigeni na lugha ya alama katika mawasiliano.
35
Sera ya Elimu na Mafunzo
Maelezo
Lugha za Kiswahili, Kiingereza, lugha nyingine za kigeni na lugha ya alama zinafundishwa kama masomo katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Pamoja na juhudi za kufundisha lugha hizo, bado kuna udhaifu wa kumudu lugha sanifu katika mawasiliano. Sehemu kubwa ya udhaifu huo inatokana na miundombinu na mbinu duni za kufundishia na matumizi madogo ya lugha sanifu katika mazingira ya kawaida.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa na inatumika kama lugha ya kwanza au ya pili miongoni mwa wananchi wengi. Lugha ya Kiswahili imekua kwa kiwango cha kimataifa ambapo inaweza kutumiwa na wananchi wengi kupata maarifa na ujuzi katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Sayansi na Teknolojia. Lugha ya Kiingereza inatumika kama lugha ya pili na ya tatu kwa baadhi ya wananchi. Kiswahili na Kiingereza ni lugha rasmi za kiofisi. Ufahamu mzuri wa Kiingereza na lugha nyingine za kigeni pia unamwezesha Mtanzania kuwa na mawasiliano na watu wa mataifa mengine na kupata elimu, ujuzi na maarifa. Aidha, lugha ya alama hutumika kufanya mawasiliano baina ya viziwi na watu wengine. Wanafunzi hawa wanashindwa kupata elimu na mafunzo kwa ufanisi kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu mahsusi wa kufundisha na kutumia lugha ya alama.
Lengo
Kujenga uwezo wa kutumia lugha mbalimbali katika mawasiliano.
36
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.2.17. Serikali itahakikisha kuwa lugha ya Kiswahili, Kiingereza na nyingine za kigeni zinafundishwa kwa ufasaha na ufanisi katika ngazi zote za elimu na mafunzo nchini ili kuleta ufahamu na umahiri kutokana na umuhimu wa lugha hizo katika masuala ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
3.2.18. Serikali itawezesha lugha ya alama na maandishi ya nukta nundu kutumika katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
Suala
Lugha ya kufundishia na kujifunzia
Maelezo
Kwa sasa, lugha za kufundishia na kujifunzia katika elimu na mafunzo ni Kiswahili na Kiingereza. Lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi ni Kiswahili. Aidha, lugha ya Kiingereza inatumika kufundishia katika baadhi ya shule.
Lugha ya Kiingereza hutumika kufundishia katika shule za sekondari, vyuo vya ualimu ngazi ya stashahada, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya juu. Aidha, lugha ya Kiswahili hutumika kufundishia katika vyuo vya mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi. Matumizi ya lugha ya Kiingereza yanazidi kupanuka ulimwenguni kutokana na utandawazi. Hali kadhalika, matumizi ya Kiswahili nchini na katika mabara mengine yameongezeka. Pia, Tanzania imeridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusiana na maendeleo na matumizi ya Kiswahili, na Tanzania kuchaguliwa kuwa makao makuu ya Taasisi ya Kuendeleza Kiswahili katika Jumuiya.
37
Sera ya Elimu na Mafunzo
Kwa hiyo, kuna umuhimu wa kuimarisha matumizi ya lugha za Kiswahili na Kiingereza kwa kuzifanya kuwa lugha za kufundishia katika ngazi mbalimbali.
Lengo
Kutumia lugha ya kiswahili katika ufundishaji
Tamko
3.2.19. Lugha ya Taifa ya Kiswahili itatumika kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo na Serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumizi ya lugha hii kuwa endelevu na yenye ufanisi katika kuwapatia walengwa elimu na mafunzo yenye tija kitaifa na kimataifa.
3.2.20. Serikali itaendelea na utaratibu wa kuimarisha matumizi ya lugha ya Kiingereza katika kufundishia na kujifunzia, katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
Suala
Upimaji, tathmini na maendeleo ya wanafunzi katika elimu na mafunzo.
Maelezo
Upimaji na tathmini katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari, vyuo vya ualimu, vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya ufundi na vyuo vya elimu ya juu hufanywa na shule, taasisi au vyuo na wakati mwingine kuratibiwa na taasisi zilizopewa dhamana hiyo. Muundo na taratibu za upimaji katika ngazi hizi umekuwa na changamoto nyingi. Changamoto mojawapo katika eneo hili ni aina ya upimaji usiozingatia malengo ya mitaala ya kujenga ujuzi, na mfumo usiohusisha kikamilifu wakuza mitaala, watekelezaji, wapimaji na wasimamizi. Pia,
38
Sera ya Elimu na Mafunzo
kutozingatiwa muundo thabiti wa upimaji kwa kujumuisha alama za maendeleo ya mwanafunzi akiwa shuleni na alama za mtihani wa mwisho unaotungwa na Baraza la Mitihani inachangia kutofikiwa kwa malengo ya mtaala husika. Aidha, mfumo wa utoaji wa alama za A, B, C, D, E, S na F zinazotolewa na Baraza la Mitihani hutofautiana mwaka hadi mwaka, na katika masomo tofauti na kutofautiana katika tafsiri baina ya shule na Baraza la Mitihani. Hali hii inasababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na elimu na mafunzo katika ngazi za juu bila sababu za msingi. Kuna umuhimu wa kuwepo kwa muundo madhubuti ili kuleta ufanisi katika mfumo wa upimaji na tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma.
Kwa upande wa upimaji na tathmini katika elimu ya ufundi na mafunzo, njia mbalimbali zinatumika ambazo hutofautiana kulingana na fani na aina ya kozi. Upimaji huo hufanywa na vyuo chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Upimaji na tathmini katika vyuo vya elimu ya juu hufanywa na vyuo vyenyewe pamoja na taasisi zinazoratibu uendeshaji wa vyuo hivyo. Aidha, vyuo vikuu vina mamlaka ya upimaji, tathmini na utoaji tuzo baada ya programu zao kupewa ithibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambayo imetoa mwongozo wa upimaji na alama kwa masomo mbalimbali.
Kutokana na umuhimu wa upimaji na tathmini katika elimu na mafunzo, hakuna budi kuwa na utaratibu wa kitaifa wa kudhibiti upimaji na tathmini katika ngazi na programu mbalimbali za elimu na mafunzo.
39
Sera ya Elimu na Mafunzo
Lengo
Kuimarisha upimaji na tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma.
Tamko
3.2.21. Serikali itaweka mfumo wa upimaji na tathmini katika elimu na mafunzo utakaozingatia vigezo vinavyotambulika vya upimaji wa kila siku wa maendeleo ya mwanafunzi na mitihani ya mwisho ya kukamilisha ngazi husika ya elimu na mafunzo kulingana na mitaala iliyopo katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
3.2.22. Serikali itaweka na kusimamia mfumo wa kitaifa wa sifa linganifu wa tuzo kwa ngazi zote za elimu na mafunzo ili kurahisisha wahitimu kuweza kujiendeleza kielimu na mafunzo.
3.3. Upatikanaji wa Fursa Mbalimbali za Elimu na Mafunzo Nchini
Suala
Fursa kwa usawa katika elimu na mafunzo
Maelezo
Fursa za elimu na mafunzo zinapatikana kwa kila Mtanzania bila ubaguzi wa jinsi, rangi, kabila, dini, ulemavu na hali ya kijamii au kipato. Ingawa fursa hizo katika elimu ya msingi zimeongezeka hadi kufikia asilimia 92 ya wanafunzi wa rika lengwa mwaka 2012, bado uandikishaji wa wanafunzi wa rika lengwa katika elimu ya sekondari ya kawaida ni asilimia 36.6 tu na asilimia 2.7 ya wanafunzi wa rika lengwa kwa sekondari ya juu. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha uwiano sawa
40
Sera ya Elimu na Mafunzo
wa uandikishaji wa wasichana kwa wavulana katika elimu ya msingi, wakati katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano ni 0.9 kwa maana ya kwamba uandikishaji wa wasichana ni mdogo ukilinganishwa na wa wavulana. Uandikishaji wa wasichana unazidi kupungua ukilinganishwa na wa wavulana katika elimu ya sekondari ya juu ambapo uwiano wa wasichana kwa wavulana ni 0.5. Hali hii inaashiria kupungua kwa ushiriki wa wasichana katika ngazi za juu za elimu. Pamoja na hayo, kumekuwa na mdondoko wa wanafunzi katika ngazi za elimu ya msingi na sekondari. Wanafunzi wengi wanaacha shule kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo ni umbali wa kutembea kwenda shuleni na kurudi, ujauzito, ndoa za utotoni, ajira za watoto, utoro, umaskini, kukosekana kwa mahitaji maalumu shuleni kwa baadhi ya wanafunzi, na baadhi ya mila na desturi zinazokinzana na utoaji wa elimu kwa watoto wa kike. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha kwamba katika shule za msingi, jumla ya wanafunzi 69,015 (wavulana 37,578 na wasichana 31,437) kati ya 8,247,172 sawa na asilimia 0.8 waliacha shule kwa sababu mbalimbali wakati kwa shule za sekondari wanafunzi walioacha shule ni 76,050 (wavulana 42,559 na wasichana 33,491) kati ya wanafunzi 1,884,272 sawa na asilimia nne (4). Pamoja na juhudi za Serikali, sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kutoa fursa za elimu kwa makundi yote, baadhi ya makundi bado hayajafikiwa kikamilifu kutokana na sababu za kijamii, kiuchumi na kijiografia. Ili kufikia malengo ya elimu na mafunzo kwa wote kuna umuhimu wa kuondoa vikwazo vinavyosababisha wanafunzi kushindwa kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika, ikiwemo changamoto zinazotokana na mahitaji maalumu kwa baadhi ya wanafunzi.
41
Sera ya Elimu na Mafunzo
Lengo
Kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanakamilisha mzunguko wa elimu na mafunzo katika ngazi husika.
Tamko
3.3.1. Serikali itaendelea kuongeza fursa anuwai za elimu na mafunzo kwa usawa kwa makundi yote ya kijamii katika ngazi zote ikiwemo watoto wenye mahitaji maalumu.
3.3.2. Serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia fursa ya wanafunzi kuendelea na masomo na kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika.
Suala
Usawa wa jinsi katika elimu na mafunzo
Maelezo
Uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi katika elimu ya msingi kwa wavulana na wasichana ni takribani 1:1; elimu ya sekondari ni 1:0.9 wakati elimu ya juu ni 1:2. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa mwendelezo wa mwanafunzi kutoka ngazi moja kwenda ngazi inayofuata kwa wasichana umekuwa ukipungua. Ingawa kiwango cha mdondoko kinaathiri wavulana na wasichana, tathmini inaonyesha kuwa wasichana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukatisha masomo hususan wanapofikia katika madarasa ya juu kuanzia darasa la tano. Halikadhalika, ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi mbalimbali za usimamizi na uongozi ni mdogo kutokana na dhana kwamba wanawake hawana uwezo sawa na wanaume. Kuna umuhimu wa kuweka usawa wa ushiriki katika fursa za elimu na mafunzo pamoja na nafasi za usimamizi na uendeshaji katika sekta ya elimu na mafunzo.
42
Sera ya Elimu na Mafunzo
Lengo
Kuwa na usawa wa kijinsi katika elimu na mafunzo
Tamko
3.3.3. Serikali kwa kushirikiana na wadau itahakikisha kuwa usawa wa kijinsi katika elimu na mafunzo unazingatiwa.
Suala
Elimu na mafunzo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo huria na masafa.
Maelezo
Serikali imeweka utaratibu wa elimu au mafunzo kwa ajili ya watoto, vijana na watu wazima waliokosa fursa katika mfumo wa kawaida, ili kujiendeleza kielimu na kumudu changamoto za maisha au kuhitimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Utaratibu huo ni pamoja na kuwepo kwa Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu na Jamii (MUKEJA) na Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA). Fursa za aina hii zinaweza kutolewa kwa ufanisi kwa kuweka miundo stahiki katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo nchini.
Elimu inaweza kutolewa vizuri zaidi endapo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na rasilimaliwatu wenye ujuzi stahiki vitatumika. Hii pia ni katika kutambua mafanikio ya kujielimisha kwa njia mbalimbali zikiwemo elimu kwa njia ya posta, elimu kwa njia ya redio, televisheni, maktaba za taifa na kisomo cha watu wazima. Kuna upungufu wa rasilimaliwatu wa kutoa elimu kwa njia ya masafa na pia vifaa vya TEHAMA ni vichache na havikidhi mahitaji ya utandawazi na ushindani pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, na hivyo, wakati
43
Sera ya Elimu na Mafunzo
mwingine kusababisha changamoto za ufanisi na viwango duni vya ubora wa elimu itolewayo.
Lengo
Kuimarisha elimu na mafunzo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo ujifunzaji huria na masafa.
Tamko
3.3.4. Serikali itaweka utaratibu na mazingira wezeshi kuhakikisha elimu na mafunzo ikiwa ni pamoja na elimu ya watu wazima inatolewa kwa ufanisi katika ngazi zote kwa njia mbalimbali ikiwemo ujifunzaji huria na masafa.
3.3.5. Serikali itaweka utaratibu na kusisitiza matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa elimu na mafunzo katika ngazi zote.
Suala
Kutambua na kuendeleza vipaji na vipawa
Maelezo
Mitaala ya sasa haitoi fursa ya kubaini na kukuza vipaji na vipawa kwa kuzingatia mahitaji na kasi ya wanafunzi kujifunza katika ngazi zote za elimu na mafunzo. Utaratibu uliopo unazingatia wale tu wenye ufaulu wa juu wa mitihani kuwa ndiyo pekee wenye vipaji. Hali hii, haitoi fursa ya kubaini, kukuza na kuendeleza vipaji vya aina mbalimbali kwa wanafunzi katika ngazi mbambali za elimu na mafunzo kama vile, muziki, ngoma, ufundi, uchoraji na michezo. Kutokana na udhaifu huu wa mitaala iliyopo, kuna haja ya kupitia mitaala hii ili izingatie wanafunzi wenye vipaji, kasi ya kujifunza, vipawa na kuwaendeleza.
44
Sera ya Elimu na Mafunzo
Lengo
Kuwa na mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatia vipaji, vipawa na kasi ya kujifunza na kutoa fursa ya kuwaendeleza.
Tamko
3.3.6. Serikali itaweka utaratibu utakaowezesha maendeleo ya wanafunzi wenye vipaji, vipawa mbalimbali, kasi tofauti na mahitaji maalumu katika kujifunza kwa ngazi zote za elimu na mafunzo.
Suala
Kuwatambua watu waliopata ujuzi bila kupitia mfumo wa elimu na mafunzo.
Maelezo
Mfumo wa elimu uliopo, hauna utaratibu wa kuwatambua watu waliopata elimu na mafunzo bila kuwa darasani au sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo; na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kujiendeleza kielimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo. Ili kujiendeleza kielimu, mfumo uliopo unahitaji vyeti vinavyotambulika kutoka shule au chuo kinachotambulika na hivyo kushindwa kutoa nafasi kwa wale walioshindwa kupata fursa hizo. Kujiendeleza kielimu ni haki ya kila Mtanzania. Elimu na mafunzo endelevu kwa maana ya elimu na mafunzo yasiyo na mwisho ni jambo ambalo Taifa halina budi kulitilia maanani ili kupata jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi. Kwa jinsi hii, ni muhimu kuwatambua na kuwapa fursa watu waliopata elimu, maarifa, ujuzi au stadi mbalimbali kujiendeleza kielimu.
45
Sera ya Elimu na Mafunzo
Lengo
Kutambua na kurasimisha maarifa, ujuzi na stadi alizopata mtu nje ya mfumo wa shule ili aweze kujielimisha kwa njia mbalimbali.
Tamko
3.3.7. Serikali itaweka utaratibu na kuimarisha utambuzi wa maarifa, ujuzi na stadi zilizopatikana nje ya mfumo wa shule ili kupanua fursa za kujiendeleza kielimu.
3.4. Mahitaji ya Rasilimaliwatu Kulingana na Vipaumbele vya Taifa
Suala
Upatikanaji wa walimu na rasilimaliwatu wengine mahiri kwa ajili ya sekta ya elimu.
Maelezo
Uhitaji wa walimu katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo katika sekta ya elimu, umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Hali hii imechangiwa na upanuzi wa sekta ya elimu pamoja na kukosekana kwa vivutio ambavyo vingewahamasisha wanataaluma mbalimbali kuingia katika fani ya ualimu na kuwabakisha humo. Aidha, kufuatia kupanuka kwa sekta nyingine nchini, baadhi ya walimu wamekuwa wakiacha kazi ya ualimu na kujiunga na sekta ambazo zinavutia zaidi kimaslahi na mazingira. Kutokana na hali hii kumekuwa na uhitaji mkubwa wa walimu katika fani mbambali hasa za ufundishaji wa stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), hisabati, sayansi na lugha. Kwa mfano, hadi kufikia Desemba 2013, mahitaji ya walimu katika maeneo mbalimbali ya sayansi na hisabati yalikuwa kama inavyooneshwa kwenye jedwali.
46
Sera ya Elimu na Mafunzo
Somo
Wanao- hitajika
Waliopo
Upungufu
Idadi
Asilimia
Agriculture
905
300
605
66.9
Physics
10,203
3,748
6,455
63.3
Computer Studies
1,108
433
675
60.9
Electrical Engineering
69
29
40
58.0
Basic Mathematics
13,478
5,896
7,582
56.3
Chemistry
10,541
4,887
5,654
53.6
Biology
11,144
5,561
5,583
50.1
Engineering Science
47
24
23
48.9
Mechanical Engineering
80
41
39
48.8
Food and Nutrition
220
120
100
45.5
Civil Engineering
100
60
40
40.0
Additional Mathematics
512
310
202
39.5
Total
48,407
21,409
26,998
55.8
Chanzo: Basic Education Statistics in Tanzania – BEST, 2013 Katika elimu ya juu, takwimu za mwaka 2012/13 zinaonesha kuwa vyuo vya elimu ya juu vinahitaji jumla ya wanataaluma 7,556 ambao wamebobea katika fani mbalimbali. Hivi sasa, vyuo hivi vina jumla ya wanataaluma 5,441 na hivyo kuwa na upungufu wa wanataaluma 2,115. Upungufu wa wahadhiri/ wanataaluma unachangia katika kuathiri ubora wa elimu ya juu nchini. Kwa hali hii, kuna haja ya kuweka mazingira bora yatakayohakikisha kwamba vijana wengi wenye umahiri wa juu wanajiunga na kubaki katika taaluma ya ualimu ili kukidhi mahitaji ya nchi katika ngazi mbalimbali za elimu na mafunzo.
Lengo
Kuwa na rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya sekta ya elimu na mafunzo.
47
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.4.1. Serikali itainua ubora wa mfumo wa ajira katika sekta ya elimu na mafunzo ili uwe mahsusi na kukidhi mahitaji, upatikanaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu na mafunzo.
Suala
Upatikanaji wa rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha katika sekta nyingine.
Maelezo
Taifa limejiwekea vipaumbele ambavyo vitaiwezesha Tanzania kufikia kiwango cha nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Vipaumbele hivyo ni pamoja na miundombinu, kilimo, viwanda, rasilimaliwatu na huduma za jamii, utalii, biashara na huduma za kifedha. Kutokana na vipaumbele hivyo, sekta ya elimu na mafunzo inatakiwa kuandaa rasilimaliwatu ya kutosha kukidhi mahitaji ya sekta za vipaumbele na mahitaji mengine kitaifa, kikanda na kimataifa. Kuna nakisi kubwa ya wataalamu walioelimika kwa kiwango cha juu wanaohitajika ili Tanzania kufikia kiwango cha nchi yenye uchumi wa kati. Ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba rasilimaliwatu ya Tanzania, kwa kiasi kikubwa ni wafanyakazi wenye ujuzi wa chini ambao ni asilimia 84, wakifuatiwa na wenye ujuzi wa kati asilimia 13 na wenye ujuzi wa juu asilimia 3. Hata hivyo, kwa nchi za kipato cha kati ngazi ya chini, ulinganifu unaonyesha kuwa nchi hizo zina wastani wa asilimia 55 ya wafanyakazi wenye ujuzi wa chini, asilimia33ujuziwakatinaasilimia12ujuziwajuu.Hivyo,Tanzania ina changamoto ya kuinua mchanganyiko wa wafanyakazi wenye ujuzi katika fani mbalimbali ili kufikia mahitaji ya rasilimaliwatu kwa nchi ya kipato cha kati kufikia mwaka 2025.
48
Sera ya Elimu na Mafunzo
Mfumo wa elimu na mafunzo wa sasa hauliwezeshi Taifa kukidhi ongezeko la mahitaji ya rasilimaliwatu kulingana na vipaumbele vya Taifa kwa sababu takwimu za mwaka 2000 hadi 2012 zinaonyesha kuwa ni wastani wa asilimia 5 tu ya wahitimu wa darasa la saba ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi kufikia elimu ya sekondari ya juu; asilimia 4.3 hujiunga na mafunzo ya ufundi stadi, asilimia 1.2 hujiunga na elimu ya ufundi ; na wastani wa asilimia 4 ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi kufikia elimu ya juu. Kwa mwenendo huo, ni dhahiri kwamba Taifa litaendelea kuwa na nakisi ya wataalamu, kama hatua madhubuti za kuongeza fursa na kuinua ubora wa elimu hazitachukuliwa.
Lengo
Kuwa na rasilimaliwatu mahiri na ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya sekta mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa.
Tamko
  1. 3.4.2.  Serikali itaweka utaratibu nyumbufu wa maendeleo ya wanafunzi kielimu na mafunzo na kufanya tathmini ya mara kwa mara ili kujua mahitaji kamili ya rasilimaliwatu na ujuzi unaohitajika ili elimu na mafunzo yanayotolewa yaweze kukidhi mahitaji.
  2. 3.4.3.  Serikali itaweka mazingira bora na kuhakikisha kuwa sekta ya elimu na mafunzo inatoa rasilimaliwatu ya kutosha na mahiri ili kukidhi mahitaji ya sekta mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa.
49
Sera ya Elimu na Mafunzo
3.5. Usimamizi na Uendeshaji Madhubuti wa Elimu na Mafunzo Nchini
Suala
Uongozi, usimamizi na uendeshaji katika sekta ya elimu na mafunzo
Maelezo
Kumekuwa na changamoto katika uzingatiaji wa majukumu na uwajibikaji katika sekta ya elimu kutokana na mfumo wa uongozi, usimamizi na uendeshaji kuanzia ngazi ya wizara zinazohusika na elimu na mafunzo, hadi ngazi ya shule, vyuo na asasi mbalimbali ambazo umeathiri ufanisi wa sekta ya elimu. Sekta ya elimu na mafunzo imekuwa ikiongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) kutokana na muundo wa wizara zilizokuwepo wakati huo pamoja na asasi zake. Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) zilikuwa zikisimamiwa na iliyokuwa Wizara Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) ilikuwa ikisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni. Mafunzo ya ufundi stadi yalikuwa yakisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya kazi. Kufuatia mabadiliko mbalimbali, na kuanzishwa kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mwaka 2006, kumekuwa na haja ya kuwa na sera inayosimamia elimu kulingana na majukumu mapya ya Wizara. Ugatuaji wa majukumu katika sekta ya elimu na mafunzo kutoka ngazi ya Serikali Kuu kwenda Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo ya usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi na sekondari umesababisha mwingiliano wa majukumu na kutowajibika.
50
Sera ya Elimu na Mafunzo
Pamoja na mabadiliko hayo, sheria, kanuni na miongozo ya uongozi, usimamizi na uendeshaji hazikufanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji. Kwa mfano, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, OWM-TAMISEMI na Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu kwa pamoja zimekuwa zikishughulikia masuala ya ajira ya walimu bila kuwa na mipaka iliyowazi na hivyo kuathiri ufanisi na uwajibikaji. Aidha, mipaka ya madaraka katika uongozi na usimamizi kati ya OWM-TAMISEMI na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haiko bayana.
Kutokana na mwingiliano huo, kuna umuhimu wa kuhuisha sheria, kanuni, miongozo na majukumu ya WyEMU na OWM- TAMISEMI ili masuala ya kisera yafanywe na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ya kiutendaji yafanywe na OWM- TAMISEMI na hivyo kuleta ufanisi na uwajibikaji.
Lengo
Kuwa na uongozi, usimamizi na uendeshaji wenye tija na uwajibikaji katika sekta ya elimu na mafunzo.
Tamko
3.5.1. Serikali itahuisha mfumo na muundo wa uongozi, usimamizi na uendeshaji katika sekta ya elimu ili uwe na tija na uwajibikaji.
3.5.2. Serikali itaweka utaratibu wa kuteua na kutambua nafasi za usimamizi wa utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa, wilaya, kata, vyuo na shule ili ziwe na hadhi maalumu katika utumishi.
3.5.3. Serikali itahakikisha maadili na haiba ya walimu na watumishi wengine yanazingatiwa katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
51
Sera ya Elimu na Mafunzo
Suala
Ushirikiano wa elimu na mafunzo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Maelezo
Elimu ya Juu ni suala la muungano, wakati ngazi nyingine za elimu siyo za muungano. Hata hivyo, sekta za Elimu Tanzania Bara na Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano katika maeneo ya mitaala na upimaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi. Hali kadhalika, katika ngazi ya elimu ya sekondari na vyuo vya ualimu kuna uhusiano katika maeneo ya mitaala, upimaji na utoaji vyeti. Kwa kuzingatia suala hilo, kuna umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kielimu baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Lengo
Kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kielimu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Tamko
3.5.4. Serikali itaimarisha ushirikiano katika elimu na mafunzo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Suala
Ushirikiano katika elimu na mafunzo kikanda na kimataifa.
Maelezo
Umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika elimu na mafunzo unazidi kuongezeka kutokana na maendeleo ya uchumi unaotegemea maarifa na ujuzi. Kwa hiyo, ushirikiano ni suala linalohitajika kwa kuwa maarifa na stadi hazina mipaka wala ukomo. Tanzania imeridhia mikataba, itifaki
52
Sera ya Elimu na Mafunzo
na maazimio mbalimbali ya kikanda na kimataifa ambayo yamechangia mafanikio yaliyopatikana nchini katika sekta ya elimu na mafunzo. Zipo changamoto mbalimbali hususan katika kurekebisha sera, sheria, mifumo na miundo ya utekelezaji ili kujumuisha masuala ya kikanda na kimataifa.
Lengo
Kuweka utaratibu wa kutekeleza mahusiano na mashirikiano ya kikanda na kimataifa katika elimu na mafunzo.
Tamko
3.5.5. Serikali itaweka muundo wa kutekeleza mahusiano na mashirikiano ya kikanda na kimataifa katika elimu na mafunzo baina ya Tanzania na nchi nyingine.
Suala
Mahitaji ya ardhi kwa maendeleo ya elimu na mafunzo.
Maelezo
Mahitaji ya ardhi kwa ajili ya upanuzi, uanzishaji na uendelezaji wa asasi za elimu na mafunzo yanaendelea kuongezeka kutokana na azma ya Serikali kupanua fursa za elimu katika ngazi zote ili kukidhi mahitaji ya mipango ya maendeleo ya Taifa. Aidha, baadhi ya asasi za elimu na mafunzo ziko kwenye ardhi ambayo haijamilikishwa kisheria. Vilevile, kumekuwepo na uvamizi wa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya asasi za elimu na mafunzo za Serikali na zisizo za Serikali. Kwa hali hiyo, asasi za elimu na mafunzo zinahitaji kumiliki ardhi ya kutosha kwa mahitaji ya sasa na maendeleo ya baadaye. Ili kulinda ardhi za asasi za elimu na mafunzo nchini zisivamiwe, kuna umuhimu kwa asasi zote za elimu na mafunzo kuwa na umiliki wa ardhi kisheria. Pia, mipango ya ardhi katika Halmashauri haijatoa
53
Sera ya Elimu na Mafunzo
kipaumbele cha kutosha katika kutenga ardhi kwa ajili ya shule, vyuo na taasisi za elimu katika ngazi zote.
Lengo
Kutenga ardhi kwa ajili ya matumizi ya elimu na mafunzo.
Tamko
3.5.6. Serikali itahakikisha kuwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya elimu na mafunzo yanazingatiwa kwenye mipango ya maendeleo ya ardhi nchini.
Suala
Mfumo wa takwimu na taarifa za elimu na mafunzo.
Maelezo
Sekta ya elimu na mafunzo ina mfumo wa kupata na kutoa takwimu za elimu na mafunzo katika asasi zake. Mfumo huo unahitaji kuwa madhubuti ili utaratibu wa ukusanyaji na utunzaji wa takwimu na taarifa uwe sahihi na wa kuaminika na takwimu kupatikana kwa wakati. Kuna kumbukumbu muhimu ambazo zimewekwa katika mpangilio tofauti tofauti na kufanya upatikanaji na matumizi yake kuwa magumu. Hatua zote za mipango ya elimu, zinahitaji taarifa zenye ubora. Kwa hiyo, mifumo ya taarifa inatakiwa iwe rahisi kutumika kwa kuhakikisha ukusanyaji, uchambuzi, uhifadhi na usambazaji wa takwimu na taarifa unakuwa fanisi. Kuwepo kwa mfumo madhubuti wa menejimenti ya data kunachangia kwa kiasi kikubwa kuleta ufanisi katika uendeshaji wa elimu na mafunzo.
Lengo
Kuwa na mfumo wa hazina data unganifu katika elimu na mafunzo.
54
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.5.7. Serikali itaimarisha mfumo wa menejimenti ya hazina data unganifu za elimu na mafunzo kwa ngazi zote.
3.6. Mfumo Endelevu wa Ugharimiaji wa Elimu na Mafunzo Nchini.
Suala
Ugharimiaji wa elimu na mafunzo.
Maelezo
Serikali inagharimia elimu na mafunzo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya elimu wa ndani na nje. Kutokana na ongezeko la mahitaji ya elimu na mafunzo, jamii pia imekuwa ikichangia katika ugharimiaji wa elimu na mafunzo kwa njia mbalimbali ikiwemo ujenzi na uendeshaji wa shule na vyuo unaofanywa kupitia sekta ya umma na binafsi. Ada pamoja na michango mingine ambayo inatolewa na wazazi na wanafunzi katika shule na vyuo vya umma na binafsi pia zimekuwa ni sehemu ya michango ya kuendesha shule na vyuo hivyo. Serikali hutenga kati ya asilimia 17 mpaka 23 ya bajeti ya Taifa kwa ajili ya elimu na mafunzo ikiwemo mikopo na ruzuku kwa ajili ya wanafunzi. Pia, fedha zinazotengwa katika bajeti ya elimu hazitoshelezi mahitaji halisi ya kuinua ubora wa elimu na mafunzo kutokana na changamoto za mfumo na muundo wa rasilimali fedha kwa ajili ya elimu. Changamoto hizo ni pamoja na fedha kutopatikana kwa wakati zinapohitajika au kutolewa pungufu kuliko kiasi kilichoidhinishwa, hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yaliyopangwa katika kipindi cha mwaka wa fedha husika. Aidha, utaratibu wa
55
Sera ya Elimu na Mafunzo
upelekaji wa fedha kwenye shule ama taasisi za elimu unahitaji kuwa bora zaidi ili kuhakikisha kuwa fedha zinazopelekwa zinafika na kutumika kwa kazi iliyokusudiwa kuliko ilivyo sasa ambapo kuna nyakati fedha zinazopatikana hutumika katika malengo tofauti. Hali hii imechangia sekta ya elimu kushindwa kutekeleza kikamilifu majukumu yake na hivyo kuathiri ufikiwaji wa malengo yaliyowekwa. Hali kadhalika, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu kiwango cha ada na michango inayotolewa katika shule na vyuo. Ada na michango hiyo katika baadhi ya shule ni kubwa kuliko matarajio na uwezo wa wananchi walio wengi na hivyo kuwa sehemu ya kero katika mfumo wa elimu na mafunzo. Katika hali hii, kuna umuhimu wa kuweka utaratibu na kubuni vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuwa na mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo. Aidha, uandaliwe utaratibu madhubuti wa kuhakikisha fedha zinafika shuleni na vyuoni na zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Lengo
Kuwa na mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo.
Tamko
3.6.1. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuimarisha mfumo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo, ikiwemo mikopo na ruzuku, ili uwe endelevu na wenye vyanzo anuai.
3.6.2. Serikali itaweka utaratibu wa ada na michango mbalimbali katika shule na vyuo binafsi ili kusimamia kwa ufanisi masuala ya ada na michango katika shule na vyuo.
56
Sera ya Elimu na Mafunzo
3.7. Mfumo wa Elimu na Mafunzo Unaozingatia Masuala Mtambuka.
Suala
Elimu ya mazingira.
Maelezo
Kuongezeka kwa idadi ya watu na shughuli mbalimbali za huduma za kijamii na za uchumi zisizozingatia taratibu zinazofaa kumesababisha uharibifu wa mazingira nchini. Hii ni pamoja na ukataji ovyo wa miti, uchafuzi wa hewa, uharibifu wa vyanzo vya maji, utupaji ovyo wa taka maji, ngumu na za sumu; na matumizi mabaya ya ardhi yaliyokithiri katika maeneo mengi. Elimu ya mazingira itiliwe mkazo zaidi katika mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote ili kupata Watanzania wenye stadi za kutunza mazingira. Elimu itolewayo shuleni na vyuoni haina budi kumjengea mwanafunzi na jamii tabia na utamaduni wa utunzaji wa mazingira.
Lengo
Kuwa na wahitimu katika ngazi zote za elimu na mafunzo wenye maarifa, stadi na utamaduni wa kutunza mazingira.
Tamko
3.7.1. Serikali itaweka utaratibu utakaohakikisha kuwa maudhui ya kutunza mazingira yanazingatiwa katika mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.
Suala
Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (VVU na UKIMWI).
Maelezo
Sekta ya elimu na mafunzo ni mojawapo ya sekta zilizoathirika na virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Maambukizi ya VVU na
57
Sera ya Elimu na Mafunzo
UKIMWI yamechangia kushuka kwa ubora wa elimu kutokana na maambukizi kuathiri walimu na wanafunzi. Kuongezeka kwa mahudhurio duni na vifo vya walimu na wanafunzi ni tishio kubwa kwa maendeleo ya elimu. VVU na UKIMWI vinaathiri kundi kubwa la rasilimaliwatu wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wenye umri unaotegemewa kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Taifa. Mojawapo ya madhara ni upotevu wa walimu wenye uzoefu na wanafunzi kushindwa kukamilisha mzunguko wa elimu na mafunzo. Hata hivyo, upatikanaji wa elimu ya kutosha ya kujikinga na kuzuia maambukizi ya VVU na UKIMWI ni changamoto kubwa kwa wanafunzi na jamii inayozunguka shule na vyuo. Aidha, kutokana na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi katika ngazi za elimu na mafunzo kumekuwa na upungufu wa washauri nasaha wenye ujuzi katika masuala ya VVU na UKIMWI na stadi za maisha.
NijukumulaWizarayaElimunaMafunzoyaUfundikushirikiana na taasisi zake pamoja na taasisi nyingine zinazohusika na VVU na UKIMWI kuhakikisha upatikanaji wa taarifa za VVU na UKIMWI katika shule na vyuo. Taarifa hizi ni pamoja na mada zisizotahiniwa zinazohusu VVU na UKIMWI katika shule na vyuo. Elimu itolewayo shuleni na vyuoni haina budi kuzingatia umuhimu wa kumwelimisha mwanafunzi katika umri mdogo ili kumjengea tabia na mwenendo stahiki kuhusu kujikinga na maambukizi ya VVU na UKIMWI, pamoja na kutoa huduma na faraja kwa walioathirika.
Lengo
Kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu na jamii ili kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI.
58
Sera ya Elimu na Mafunzo
Tamko
3.7.2. Serikali itajumuisha stadi za kujikinga na VVU na UKIMWI katika mitaala ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.
Suala
Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika elimu na mafunzo.
Maelezo
Sekta ya elimu na mafunzo ni mojawapo ya maeneo muhimu ya uwekezaji kwa njia ya ubia baina ya sekta ya umma na binafsi. Sekta ya elimu ina mahitaji makubwa yakiwemo ya maabara za sayansi, karakana, madarasa, mabweni na nyumba za walimu pamoja na miundombinu mingine muhimu ya ustawi wa wanafunzi na walimu katika shule na vyuo.
Kwa kutambua ufinyu wa rasilimali za umma na mchango wa sekta binafsi, kuna umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi katika sekta ya elimu ili kutumia rasilimali na fursa za sekta binafsi kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji kwa njia ya ubia.
Lengo
Kuongeza uwezo wa sekta ya elimu na mafunzo katika kupanua na kuimarisha miundombinu na huduma mbalimbali katika ngazi zote za elimu na mafunzo
Tamko
3.7.3. Serikali itaimarisha ubia baina ya sekta ya umma na binafsi katika upatikanaji wa miundombinu ya kisasa na huduma mbalimbali katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
3.7.4. Serikali itapanua wigo na kuimarisha ushiriki fanisi wa wadau mbalimbali katika sekta ya elimu na mafunzo katika ngazi zote.
59
Sera ya Elimu na Mafunzo
SURA YA NNE 4.0. MUUNDO WA KISHERIA
4.1 Utangulizi
Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utazingatia muundo wa kisheria utakaowawezesha wahusika kutekeleza majukumu yao. Kwa mujibu wa Sera hii, majukumu ya kila sehemu ya sekta hayana budi yawekwe wazi ili kuondoa mkanganyiko na migongano ambayo imekuwa ikijitokeza katika usimamiaji na utekelezaji wa masuala mbalimbali ya elimu. Aidha, taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na zitakazoundwa zitatekeleza masuala ya elimu na kuwajibika kwa Wizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo. Hali kadhalika, sekta za umma na binafsi zinazoshughulikia utoaji wa elimu na mafunzo zitatakiwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa katika kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo.
4.2 Sheria za kusimamia elimu na mafunzo
Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utafuata sheria mbalimbali. Sheria zilizopo zitarekebishwa ili ziendane na mahitaji ya matamko ya Sera hii. Baadhi ya sheria zitakazorekebishwa ni pamoja na Sheria za Serikali za Mitaa (Sura ya 287 na Sura ya 288 ya Sheria za Tanzania) ili ziweze kukidhi mahitaji ya ugatuaji wa elimu ya awali, elimu ya msingi na elimu ya sekondari. Mabadiliko ya sheria hizi yatalenga katika kuhakikisha kwamba kunakuwa na usimamizi na uendeshaji thabiti wa elimumsingi na sekondari katika ngazi mbalimbali za OWM-TAMISEMI. Aidha, sheria nyingine ambazo hazikidhi mahitaji ya utekelezaji wa sera hii zitafutwa au kurekebishwa. Baadhi ya sheria hizo ni Sheria ya Elimu Sura ya 353, Sheria ya Baraza la Mitihani la Tanzania Sura ya 107, Sheria ya Taasisi
60
Sera ya Elimu na Mafunzo
ya Elimu Tanzania Sura ya142, Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Sura ya 178, Sheria ya Vyuo Vikuu Sura ya 346, Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Sura ya 129, Sheria ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Sura ya 82 , Sheria ya Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Sura ya 102, Sheria ya Mfuko wa Elimu Sura ya 412, na Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Sura ya 139. Vilevile, sheria nyingine mpya zinaweza kutungwa kufuatana na mahitaji ili kukidhi maelekezo na matamko mapya ya sera ambayo hayawezi kutekelezwa kwa sheria zilizopo. Baadhi ya sheria zitakazotungwa ni pamoja na sheria ya elimumsingi na sekondari. Sheria hii itaelekeza masuala mbalimbali ya elimumsingi na sekondari ikiwemo mitaala na upimaji wa kitaifa katika ngazi hizi.
61
Sera ya Elimu na Mafunzo
SURA YA TANO
5.0 MUUNDO WA KITAASISI NA UFUATILIAJI NA TATHMINI
5.1. Utangulizi
Majukumu ya Wizara yenye dhamana ya Elimu na Mafunzo
ni:
  1. (i)  Kutunga Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi
    zote;
  2. (ii)  Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa elimu
    na mafunzo katika ngazi zote;
  3. (iii)  Kuweka na kufuatilia utekelezaji wa mipango na bajeti ya maendeleo ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya ufundi (ikiwemo ualimu) na elimu ya juu;
  4. (iv)  Kufuatilia na kufanya tathmini ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya ufundi na elimu ya juu;
  5. (v)  Kujenga uwezo wa Wizara, taasisi na vyombo vilivyo chini ya Wizara kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake;
  6. (vi)  Kutumia matokeo ya tathmini, utafiti na taarifa mbalimbali zinazohusu hali halisi ya utoaji wa elimu na mafunzo ili Wizara iweze kutoa maamuzi yenye tija na yatakayoongeza ufanisi katika utekelezaji wa mkakati wa sera;
  7. (vii)  Kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya ufundi na elimu ya juu; na
  8. (viii)  Kulinda uhuru na kujenga uwezo wa vyombo vya ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu nchini.
62
Sera ya Elimu na Mafunzo
Kwa upande wa OWM-TAMISEMI itakuwa na jukumu la kuandaa mipango, bajeti, usimamizi na uendeshaji wa shule za elimumsingi na sekondari na kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango vya ubora wa elimu vinavyotambulika kikanda na kimataifa. Hali kadhalika, , Wizara pamoja na taasisi nyingine zenye kuhusika na utoaji wa elimu na mafunzo zitawajibika kuhakikisha uwepo wa mipango, bajeti, usimamizi na uendeshaji bora wa elimu katika maeneo yao. Aidha, utekelezaji wa Sera hii unahitaji muundo mahsusi wa kitaasisi katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi za chini za utoaji wa elimu na mafunzo.
5.2. Ngazi ya Taifa
Katika kutekeleza sera ya elimu na mafunzo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itakuwa na muundo wa kitaasisi utakaojumuisha idara za utafiti na kumshauri Waziri juu ya maendeleo ya Sera katika elimu ya awali, elimumsingi sekondari, elimu ya ualimu, elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya juu na mfumo wa Tuzo wa Taifa na mahusiano ya kimataifa kuhusu elimu na mafunzo nchini. Idara nyingine zitakuwepo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za ofisi za umma.
Taasisi na Vyuo vilivyo chini ya wizara vitawajibika katika majukumu ambayo vitapangiwa na wizara kwa mujibu wa sheria na kutoa taarifa za utekelezaji kulingana na taratibu. Wizara, taasisi, mashirika ya umma na binafsi yenye shule, vyuo au taasisi za elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali zitawajibika kuwasilisha taarifa na mipango iliyopitishwa na shule, vyuo au taasisi hizo kwa mujibu wa taratibu ili kuiwezesha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoa taarifa juu ya mipango na maendeleo ya elimu na mafunzo
63
Sera ya Elimu na Mafunzo
kwa ujumla. Wadau wote wa maendeleo wanakaribishwa kwa dhati kushiriki katika masuala mbalimbali ya elimu na ufundi nchini. Katika kufanikisha hili, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaweka utaratibu ambao utawapa fursa wadau wa maendeleo kuchangia kwa ufanisi maendeleo ya elimu na mafunzo nchini.
Pia mamlaka za kusimamia elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali zitakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake ili kuleta tija katika maendeleo ya elimu nchini. Mamlaka hizi ni pamoja na Mamlaka ya Ithibati na Uthibiti wa ubora wa Elimumsingi na Sekondari, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu, Taasisi ya Elimu Mtandao Dakawa na nyingine zitakazoundwa kulingana na mahitaji. Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM - TAMISEMI zitashirikiana na wizara, taasisi na wadau wengine wanaojihusisha na utoaji wa elimu na mafunzo nchini. Ushirikiano huo utahusu uchambuzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo, kuweka viwango na kuandaa sheria, kanuni, miongozo na taratibu za utekelezaji wa Sera, kuandaa mipango mikuu ya elimu na mafunzo, kufuatilia, kupima na kutathmini utekelezaji wake.
Kwa upande wa OWM-TAMISEMI, kutakuwa na Ofisi ya Mkuu wa Elimu OWM-TAMISEMI ambayo itasaidiwa na idara za elimu ya awali, elimumsingi, sekondari, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Idara hizi zitawajibika kuwa na wataalamu wenye ujuzi wa masuala ya mipango ya elimu ya awali, elimumsingi na sekondari pamoja na masuala yanayohusu elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi, ili kupanga, kusimamia na kutekeleza ipasavyo majukumu ya OWM-TAMISEMI katika elimu na mafunzo. Idara nyingine za
64
Sera ya Elimu na Mafunzo
OWM-TAMISEMI zitaendelea kuwepo au kuundwa kulingana na majukumu mengine ya OWM-TAMISEMI.
5.3. Ngazi ya Mkoa
Jukumu la usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi ya mkoa litakuwa la Afisa Elimu Mkoa. Afisa Elimu Mkoa atashauri kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika mkoa na kutoa mrejesho na ushauri kwa OWM-TAMISEMI kuhusu maendeleo ya elimu na mafunzo katika ujumla wake.
5.4. Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
Mamlaka za Serikali za Mitaa zitahusika katika uanzishaji, usimamizi na uendeshaji wa shule za elimu ya awali, elimumsingi na sekondari na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa Katibu Tawala wa Wilaya husika. Katika ngazi hii kutakuwa na Afisa Elimu anayeshughulikia Shule za Elimu ya Awali na Elimumsingi na Afisa Elimu anayeshughulikia Shule za Sekondari. Aidha, Maafisa Elimu wa Halmashauri watasimamia na kuratibu utekelezaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi katika maeneo wanayosimamia.
Wote watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa kufuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi na uendeshaji wa shule za Serikali na zisizo za Serikali. Katika kutekeleza jukumu hilo, Afisa Elimu atatakiwa kushirikiana na viongozi wengine wa Halmashauri, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali, mashirika na taasisi za Serikali na zisizo za Serikali katika ngazi ya Halmashauri. Maafisa Elimu wa Halmashauri pia watawajibika kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shule zilizoko katika Halmashauri zao kulingana na miongozo itakayotolewa na chombo cha Ithibati na uthibiti
65
Sera ya Elimu na Mafunzo
wa Elimumsingi na Sekondari. Pia kila Halmashauri itakuwa na chombo ambacho kitawajibika katika kutoa ushauri wa masuala ya elimu ya awali, elimumsingi, sekondari na elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi pamoja na mambo mengine yanayohusu elimu katika Halmashauri husika. Chombo hicho kitakuwa na wajumbe ambao wana uwezo na sifa stahiki katika kutoa ushauri katika masuala ya elimu na mafunzo kwenye ngazi hiyo.
Kutakuwa pia na Maafisa Uhakiki wa Ubora na Viwango vya Elimu na Mafunzo katika ngazi ya Halmashauri. Jukumu la Maafisa hawa katika ngazi hii litakuwa ni kuhakikisha shule zinaendeshwa kwa kuzingatia viwango vya uendeshaji na kuzikagua kulingana na utaratibu uliowekwa ili kuhakikisha kwamba upungufu unaojitokeza unafanyiwa kazi kwa haraka na hivyo kufanya kiwango cha elimu na mafunzo kukua.
5.5. Ngazi ya Kata
Katika ngazi ya Kata, utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo utasimamiwa na Afisa Elimu Kata ambaye atakuwa mratibu wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa Shule za Serikali na zisizo za Serikali katika ngazi ya shule za awali na elimumsingi, elimu ya sekondari, elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi. Afisa Elimu Kata atakuwa pia mkaguzi aliye jirani na shule kwa shule zilizoko katika kata yake na atawajibika kwa Afisa Elimu wa Halmashauri. Pia kila kata itakuwa na chombo cha ushauri wa elimu ambacho kitawajibika katika kutoa ushauri wa masuala ya elimu ya awali, elimumsingi na sekondari pamoja na masuala mengine yanayohusu elimu katika kata husika. Chombo hicho kitakuwa na wajumbe ambao wana uwezo na sifa stahiki katika kutoa ushauri katika masuala ya elimu na mafunzo. Kutakuwa pia na Afisa Uhakiki wa Ubora na Viwango vya Elimu na Mafunzo katika ngazi ya Kata. Idadi ya maafisa hawa itategemea idadi
66
Sera ya Elimu na Mafunzo
ya shule katika Kata husika. Jukumu la Maafisa hawa litakuwa kukagua shule mara kwa mara na ili kuhakikisha kuwa shule zinaendeshwa kwa zinazingatia miongozo ya viwango vya uendeshaji na kuhakikisha kwamba upungufu unaojitokeza unafanyiwa kazi kwa haraka, na hivyo kufanya kiwango cha elimu na mafunzo kukua.
5.6. Ngazi ya Shule na Vyuo
Wakuu wa shule za elimumsingi na sekondari watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika ngazi za shule na watawajibika kutoa taarifa za utekelezaji kwachombo kilichopewa majukumu ya kuangalia uongozi, mipango ya maendeleo ya shule, nidhamu na fedha katika shule/vyuo husika na hatimaye kwa Afisa Elimu Kata.
Wakuu wa vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi, elimu ya ufundi (vikiwemo vya ualimu na uongozi wa elimu), na vyuo vya elimu ya juu watasimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo katika vyuo vyao na kutoa taarifa za utekelezaji kwa mamlaka zilizo juu yao kwa mujibu wa sheria zinazoongoza elimu katika ngazi husika. Viongozi hawa watawajibika pia kuhakikisha kwamba shule na vyuo wanavyoviongoza vina mifumo stahiki ya ndani ya ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ama shuleni au vyuoni humo. Mifumo ya ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu na mafunzo iliyopo katika ngazi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itawajibika kufanya uhakiki wa ubora wa mifumo hii ya ndani wakati wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
5.7. Ufuatiliaji na Tathmini
Ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ni jukumu la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, OWM-TAMISEMI, na mamlaka zilizopo katika kila eneo la sekta ya elimu na mafunzo. Hata hivyo, ufuatiliaji na tathmini
67
Sera ya Elimu na Mafunzo
utategemea juhudi za pamoja na ushiriki wa karibu baina ya wizara mbalimbali, mashirika na taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, washirika wa maendeleo wa ndani na nje, jamii na wadau wengine wa elimu na mafunzo.
Utekelezaji wa matamko yaliyoainishwa katika Sera utaenda sambamba na mkakati wa utekelezaji wa Sera. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itakusanya, kuunganisha na kuchambua taarifa za utekelezaji wa maeneo mbalimbali ya Sera. Wadau wote wanawajibika kutoa taarifa stahiki kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili kufanikisha jukumu lake la kufuatilia na kutathmini maendeleo ya elimu na mafunzo nchini.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa kushirikiana na wadau wengine itakuwa na majukumu ya ufuatiliaji na tathmini ikiwemo kuweka viashiria, vigezo na muda wa tathmini. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na wadau itaweka Mpango Maalumu wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera ya Elimu na Mafunzo.
5.8. Hitimisho
Madhumuni ya Sera hii ni kutoa mwongozo wa jumla wa uendeshaji wa elimu na mafunzo kwa mtazamo wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, mipango na mikakati ya maendeleo ya Taifa, na mabadiliko ya ulimwengu hususan katika uchumi, sayansi na teknolojia ili Taifa liweze kufikia lengo la kuwa na uchumi unaoendeshwa na elimu na ujuzi na kulifanya liwe moja ya mataifa yaliyo na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Sera hii pia imezingatia masuala mtambuka ili kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa.
Elimu bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa inawezekana, wote tutekeleze wajibu wetu.
68